Wamasai Ngorongoro wamkabidhi ripoti Waziri Mkuu, ni maoni yao kuhusu Ngorongoro wanayoitaka na sio ya wataalam

Na Queen Lema, Arusha

Viongozi wa kimila kutoka katika tarafa za loliondo na ngorongoro wamefanikiwa kuwasilisha ripoti maalumu  ya mapendekezo ya maoni ya wananchi Kamati hiyo imewasilisha taarifa hiyo hivi karibuni kwa waziri mkuu Kasimu Majaliwa 


Akiongea na vyombo vya habari mapema leo Kiongozi wa kimila (Lagwanani) Bw Metui ole shaudo alisema kuwa Ripoti hiyo imebeba mapendekezo na maoni ya wananchi wa tarafa hizo.Alidai kuwa moja ya maendekezo ambayo ipo katika ripoti hiyo ni uwepo wa Ngorongoro ambayo wanaitaka na sio ile ambayo wataalamu wanaitaka 


"Tumeweka Ripoti kwa kukusanya maoni ya wananchi wote na mapendekezo ambayo tunaitaka sanjari na uhalisia"alisema 


Naye mjumbe wa kamati hiyo Bi Mageth  Kaisori alisema kuwa hapo awali kulikiwa na taarifa za ongezeko la watu na mifugo 


Kaisori alisema kuwa kuna taarifa ambazo zinasemwa mtaani lakini sio kweli kabisa 


"Kwa mfano inasemekana Ngorongoro hakuna tena msitu wakati mpaka asubui ya Leo nimepigiwa simu kuwa tembo wamezuia watoto,nataka kusema kuwa hata hao tembo wameongezeka "aliongeza Kaisori


Wakati mwenyekiti wa baraza la wafugaji bw Edward Maura  Alisema kuwa wao wanamuomba sana Raisi Samia Suluhu Aweze kuangalia Ripoti hiyo lakini hata kuifanyia kazi kwa wepesi 


Alidai kuwa kwa kipindi hiki cha kuelekea kiangazi huwa wanateswa sana na wahahifadhi hali ambayo inasababisha hata mifugo yao kufa

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post