NAIBU MEYA WA MARYLAND, USA ATEMBELEA JIJI LA ARUSHA.

Naibu Meya wa Mji wa Maryland, USA Mhe. Ron Sitoula akiwa na Naibu Meya wa halmshauri ya Jiji la Arusha Veronica Mwelange.
Naibu Meya wa Mji wa Maryland, USA Mhe. Ron Sitoula na ujumbe wake wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Meya wa Jiji la Arusha Veronica Mwelange, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji Dkt Onesmo Mandike pamoja na baadhi ya watumishi wa halmshauri.

 

Na Zulfa Mfinanga, Arusha.


Naibu Meya wa Mji wa Maryland, USA, Ron Sitoula, atembelea ofisi ya Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Mhe. Maximilian Iranghe na kupokelewa na wenyeji wake ambao ni Naibu Meya Veronica Mwelange, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji Dkt Onesmo Mandike pamoja na baadhi ya watumishi wa halmshauri.


Mhe. Sitoula amesema ziara hiyo imetokana na ziara yake binafsi na hivyo kuamua kumtembelea Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha ili kujadiliana mambo mbalimbali yanayoshabihiana kati ya halmashauri ya Jiji la Arusha na Mji wa Maryland.


Mhe. Sitoula amesema amefurahishwa na mapokezi aliyofanyiwa na wenyeji wake ikiwa ni pamoja na kuona jinsi halmashauri ya Jiji la Arusha imejipanga katika kuwaletea wananchi wake maendeleo kwa kuyawezesha  kiuchumi makundi ya vijana na wanawake, utunzaji wa mazingira na ulipaji wa kodi kwa hiari.


“Kabla ya kuondoka ningependa kujadiliana na Mstahiki Meya mambo kadhaa yanayoshabihiana kati ya halmashauri ya Jiji la Arusha na Mji wangu, lakini pia kujifunza mambo mengine nitakayobaini hapa ili kuendelea kukuza urafiki na uhusiano kati ya halmashauri hizi” Alisema Mhe. Sitoula.


Akizungumza na wageni hao, Kaimu Mkurugenzi Dkt. Mandike amesema halmashauri ya Jiji la Arusha inashirikisha wananchi kikamilifu katika mbalimbali za maendeleo ikiwemo kampeni ya utunzaji wa mazingira, ulipaji kodi kwa hiari pamoja na kuwawezesha wananchi kiuchumi jambo linaloifanya halmashauri kukua kwa kasi kimaendeleo.


Mhe. Sitoula ameahidi kurudi kesho kwa ajili ya kuonana na Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Mhe. Maximilian Iranghe kwani wakati wa ujio wao hawakufanikiwa kuonana naye kwa sababu ya kuwa nje ya nchi kikazi.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post