Mawakili wa Serikali waokoa trilioni 10

Wakili Mkuu wa Serikali Gabriel Malata

Na Mwandishi Wetu, Arusha

Ofisi ya wakili mkuu wa Serikali imefanikiwa kuisaidia Serikali kuendesha mashauri ya madai na usuluishi na kuokoa kiasi cha Trilioni 10 katika mashauri hayo. Takwimu hizo ni tangu ilipoanzishwa ofisi hiyo  mwaka 2018.


Hayo yameelezwa jana jijini hapa na Bi Mary Makondo Katibu mkuu wizara ya katiba na sheria wakati akifungua mafunzo ya mawakili wa Serikali, yaliyoandaliwa na ofisi ya wakili mkuu wa serikali.


Makondo alisema kuwa ofisi hiyo toka kuanzishwa kwake imekuwa na msaada mkubwa sana kwa kuwa imekuwa ikileta usuluishi lakini hata suluhu juu ya madai mbalimbali.


"Kwa kweli nataka niwaambie kuwa mmefanya jambo kubwa sana na mnastaili pongezu kubwa sana kwa sababu hizi fedha ni nyingi na  Kama hamkusimama ipasavyo  leo zingekuwa zimepotea"aliongeza Makondo


Aidha atika aliitaka ofisi hiyo kuendelea kufanya kazi kwa bidii sana sanjari na kusimamia maslahi ya taifa.


Aliwataka washiriki wa semina hiyo kuhakikisha wanaitumia elimu ambayo wataipata kwenye semina hiyo kwenye kazi zao ili kuendelea kuokoa zaidi ya fedha.Naye wakili mkuu wa serikali Gabriel Malata amesema ofisi yake imekuwa mstari wa mbele katika kutetea maslahi ya taifa hususani kwenye sekta ya uchumi.


Akiongelea sakata hilo la kuokoa Trilioni 10 alisema kuwa wamepambana sana ili kuokoa kiasi hicho na endapo Kama wangeshindwa basi wangelazimika kulipa wadai 


Mbali na hayo alisema kuwa bado wanakabiliwa na mambo mbalimbali ikiwemo ukosefu wa watumishi wenye stadi maalumu


Nao washiriki wa semina hiyo walidai kuwa wanashukuru ofisi hiyo kuandaa mafunzo ya siku 4  ambapo elimu watakayoipata itawasaidia sana kuongeza ufanisi  katika kazi zao hasa za usuluishi

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post