Breaking News: Waandishi wa habari wapiga mawe na watu wasiojulikana

N Mwandishi Wetu, Arusha

Waandishi wa Habari kutoka vyombo vya habari mbalimbali Mkoani Arusha wametimuliwa kwa kupigwa na mawe ambayo hayajulikani yanapotokea katika Kijiji cha Kiwawa Kata ya Imbasei Wilayani Arumeru Mkoani Arusha.

Tukio hilo limetokea baada ya Waandishi hao kufika kwenye eneo hilo kwa lengo la kufuatilia taharuki ya Wananchi kupigwa kwa mawe yanayohisiwa kurushwa na Mizimu.


Katika tukio hilo Mwandishi wa GADI TV amejeruhiwa sehemu ya kichwani  kwa kupigwa na jiwe huku mwandishi GLOBAL TV akijeruhiwa mkono wake wa kushoto.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post