Rc Katavi awaweka kikaangoni Wakurugenzi, atoa maagizo mazito

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko akipokea maelezo kutoka kwa  Mkuu wa Shule ya Sekondari Kasimba Paulo Shibon  ambae hayupo pichani juu ya Maendeleo ya  Ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Kawalyowa  inayojengwa ili kupunguza msongamano wa wanafunzi katika shule ya Sekondari Kasimba Mkoa wa Katavi

Mkuu  wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko akikagua Maendeleo ya Mradi wa Ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari Kawalyowa iliyopo Kata ya Ilembo Manispaa ya Mpanda ambapo amewaagiza Wakurugenzi kuhakikisha miradi yote inakamilika kwa wakati na Halmashauri itakayo shindwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake

 

Na Mwandishi Wetu, Katavi

Mkuu wa Mkoa wa Katavi  Mwanamvua Mrindoko amewaagiza Wakurugenzi wote wa Halmashauri zilizopo katika Mkoa wa Katavi kuhakikisha fedha zilizopo kwenye Halmashauri zao za miradi ya Maendeleo zinatumika kukamilisha miradi husika kabla ya mwaka mpya wa fedha 2022/2023 kuanza na Halmashauri itakayo sababisha fedha kurudishwa hazina itachukuliwa hatua.


Maagizo hayo ameyatoa alipokuwa kwenye ziara ya  kukagua Ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari ya Kawalyowa inayojengwa  ili kupunguza msongamano wa wanafunzi kwenye Sekondari ya Kata ya Ilembo .


Amesema kwa Halmashauri zote za Mkoa wa Katavi  na miradi yote ambayo imepata fedha katika mwaka wa fedha 2021/ 2022 haitakiwa kuvuka na fedha za miradi  na kwa maana hiyo miradi  ambayo inamaelekezo mahususi  kama vile miradi ya fedha za IMF   inatakiwa iwe imekamilika.


Amebainisha miradi yote ya Shule mpya za Sekondari za Kata  inatakiwa kukamilika Mei 31,2022 lakini miradi mingine yote ambayo haina maelekezo maalumu  inatakiwa kabla ya  Juni 30,2022 iwe imekamilika .


Amesisiza kuwa  maelekezo hayo yatekelezwe katika Halmashauri zote za Mkoa wa Katavi na aliwataka Wakuu wa Wilaya kusimamia maagizo hayo na hataki  Halmashauri yoyote kuvuka na fedha za miradi  kwani wananchi wanayo mahitaji ya  miradi inayotekelezwa kupitia fedha hizo.


Aidha amesisitiza kuwa hata mvumilia Mkurugenzi yoyote yule atakae chelewesha Ujenzi wa miradi anataka  kuona miradi inakamilika kwa wakati  ili kutimiza adhima ya Serikali ya kuwasogezea wananchi huduma karibu  ili wapate huduma kwa haraka.


Pia alisema hata sita kumchukulia hatua Mkurugenzi yoyote wa Halmashauri ambae Halmashauri yake itafanya  uzembe katika  usimamizi  na matumizi ya fedha za miradi na kushindwa kukamilisha miradi kwa wakati na fedha kurudi Hazina .


Aidha Mrindoko aliwaondoa wasiwasi wananchi wa Mkoa wa Katavi kutokana na sintofahamu baada ya kutokea mauwaji ya mtu  mmoja hivi karibuni kuwa kuna mpango umepangwa wakufanya  mauwaji ya watu ndani ya Mkoa wa Katavi jambo hilo halina ukweli wowote.


Hivyo amewahakikishia wananchi wa Mkoa wa Katavi kuwa   Mkoa upo salama na wananchi waendelea kufanya kazi zao kama kawaida anaekwenda shambani aende kama kawaida na anaefanya biashara afanye bila mashaka  kwani Mkoa upo salama na shwari.


Nae Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda  Deodatus Kangu alisema kuwa wamepokea maelekezo ya Mkuu wa Mkoa watayatekeleza kama walivyo agizwa na Mkuu wa Mkoa Mwanamvua Mrindoko.


Alisema miradi yote inayotekelezwa kwenye Halmashauri watahakikisha inakamika kabla ya June 30 mwaka huu kama ilivyo  ilekezwa

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post