JENIFER ALPHAYO:-MWANAMKE ALIYEAMUA KUACHA KAZI SERIKALINI NA KUAMUA KUJIAJIRI

Jenifer akiwa ofisini kwake


Na Pamela Mollel,Arusha 


"Nilikuwa nimeajiriwa serikalini na nilifanya kazi takribani miaka 20, lakini binafsi nilijiwekea malengo kwamba nikifikisha miaka 40 lazima nijiajiri Mimi mwenyewe".


Hayo si maneno ya mwingine bali ni Jenifer Alphayo mjasiriamali ambaye kwa sasa amefanikiwa kufungua kampuni yake iitwayo *African* *Wear & Design* inayojihusisha na masuala ya ushonaji (Tailoring) iliyo na ofisi zake Moshono nje kidogo ya jiji la Arusha


Jenifer anaeleza kwamba kwa sasa anamshukuru Mungu anaweza kutengeneza fedha kila siku na sio kusubiria mwisho wa mwezi apokee mshahara.


"Namshukuru Mungu kwa sasa naweza kushika pesa kila siku tofauti na hapo awali ambapo nilitegemea kushika pesa mwisho wa mwezi pekee" anaeleza Jenifer


Jenifer anabainisha kwamba alianza kufungua biashara yake mnamo mwaka 2000 ambapo alianza na mtaji wa kiasi cha sh,5 milioni.


Anasema kwamba kwa sasa amefanikiwa kuwa na mtaji wa zaidi ya sh,40 milioni kupitia biashara anazofanya  na kutengeneza ajira za vijana 13.


"Kwa sasa tuna mtaji zaidi na sh,40 milioni na nimefanikiwa kutoa ajira kwa zaidi ya vijana 13 " anaeleza Jenifer


Jenifer anaelezea ukuaji wa soko la ushonaji hapa nchini na kubainisha kwamba pamoja na ukuaji huo lakini ni lazima ujitofautishe na kuwa mbunifu ili kufanikiwa kuliteka  soko hilo.


Anasema kwamba anaishukuru serikali chini ya *Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia *Suluhu Hassan* kwa kuonyesha dalili  za kuwajali wajasiriamali.


"Soko la ushonaji linakua kwa sasa lakini ili uweze kufanikiwa ni lazima ujitofautishe na kuwa mbunifu " anasema Jenifer mama wa watoto watatu 


Anafafanua kwamba anatengeneza nguo za mitindo mbalimbali kupitia bidhaa aina ya vitenge ambavyo huagiza kutoka nchi za Afrika Magharibi ambazo ni Mali,Ghana na ,Ivory Coast na kusisitiza vitenge hivyo vina  soka kubwa tofauti na vitenge wanavyonunua hapa nchini .


Hatahivyo,anabainisha changamoto kuu anayokutana nayo ni suala la kukatika umeme Mara kwa Mara.


Jenifer anafafanua kwamba analazimika kutumia jenereta ambayo ni ghali  ili kukamilisha order za watu.


"Suala la kukatika kwa umeme Mara kwa Mara ni changamoto kubwa sana kwetu kwa kuwa nalazimika kutumia umeme wa jenereta na mafuta ni ghali sana tunaumia sana mteja hawezi kukuelewa kama umepata changamoto ya umeme yeye amekulipa pesa ukamilishe kazi yake kwa muda mliokubaliana" anafafanua Jenifer ambaye hivi karibuni aliibuka kuwa mshindi wa tuzo ya Malkia wa Mkoa wa Arusha 2022 katika nyanja ya Ushonaji 


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post