Wakulima watakiwa kutumia maonyesho ya Tanz food kukuza teknolojia ya kilimo

Washiriki kutoka katika Bandari ya Tanga wakihudumia wateja katika banda lao

Na Queen Lema, Arusha

 Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela amewataka vijana na watanzania wa mikoa ya jirani kutumia maonyesho ya tanz food 2022   ili kupata elimu na teknolojia  za kujifunza fursa za kujiajiri.


Mongela ameyasema hayo wakati wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya Kilimo ya Tanz food 2022 yanayofanyika kwa siku tatu katika viwanja vya magereza kisongo jijini Arusha.


Amesema kuwa kupitia maonyesho hayo ya siku tatu watanzania na vijana wanapaswa kuyatumia ili wajifunze mbinu na teknolojia za kilimo bora.


Kwa upande wake mratibu wa maonyesho hayo ambae Ni  mkurugenzi wa kampuni ya  kilifea production company LTD  Dominic shoo amesema kuwa maonyesho hayo  yatakuwa yanafanyika kila mwaka na lengo lake Ni kwa ajili ya kuwashirikisha Wakulima na kutangaza mazao yao.


Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Taha  Jackline Mkindi amesema kuwa kazi yao kubwa ni kuendeleza sekta hiyo hapa nchini.Wakizungumza kwa niaba ya washiriki wa maonyesho hayo mhandisi Hamisi Kipalo kutoka bandari ya Tanga amesema kuwa  wanaendelea na  Mradi wa uboreshaji wa bandari  kwa awamu ya pili  kwa ujenzi wa gati namba 1 na 2 lenye urefu wa mita 450 ambao unatekelezwa na mkandarasi kutoka China akisimamiwa na mhandisi mshauri  kampuni ya  Niras  kutoka Denmark akishirikiana na kampuni ya kitanzania ya Anova.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post