Nchi za EAC zatakiwa kupunguza kodi vifaa vya nishati ya umeme

John Kioli mwenyekiti wa mashirika ya kufatilia athari za mabadiliko ya tabia nchi Kenya

 

Mwandishi wetu Arusha 


Mtandao wa mashirika yasiyo ya kiserikali katika nchi za Afrika vya Mashariki ambayo yanajumuisha na masuala ya nishati yamezitaka serikali za Afrika Mashariki kupunguza kodi vifaa vya Nishati ili kupunguza tatizo la nishati hasa vijijini.Mratibu wa mtandao  kutoka taasisi ya ACCESS,Grace Ronoh  ametoa wito huo leo katika mkutano wa taasisi hizo uliofanyika jijini Arusha na kushirikisha mashirika yasiyo ya kiserikali kutoka Kenya,Uganda na Tanzania.


Ronoh amesema bado serikali za Afrika Mashariki zinatisha kodi kubwa kwa vifaa vya nishati hali ambayo inachangia gharama za wananchi kupata nishati endelevu kubwa kubwa.


Mwenyekiti na shirika la kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi nchini Kenya(KCCWG)John Kioli amesema  kutokana na gharama kubwa za vifaa vya nishati bado asilimia 80 ya wakazi wa Afrika Mashariki wanatumia mkaa na kuni .


"Bado vifaa vya umeme wa jua bei ipo juu lakini hata ambavyo bei imepunguzwa havikai hata mwezi mmoja"amesema.


Mkurugenzi wa shirika masuala ya mazingira na nishati la FEMAPO,Mathias Lyamunda amesema wanashauri nchi za EAC kutekeleza malengo ya milenia kuhakikisha jamii inapata nishati kwa bei nafuu.


Amesema licha ya Tanzania kufanya vizuri katika usambazaji umeme vijijini lakini bado kuna changamoto ya kudhibiti matumizi ya mkaa na kuni ambavyo vinaathari za kiafya na mazingira.


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post