Mvua zakatiza mawasiliano kata 5 Ludewa

 A Mwandishi Wetu, NJOMBE 


Wakazi Kutoka kata 5 za tarafa ya Mwambao wilayani Ludewa Mkoani Njombe wameshindwa kuendelea na safari zao za kila siku kwa zaidi ya siku nne baada ya mvua kubwa zinazoendelea Kunyesha kusababisha mmomonyoko mkubwa wa ardhi katika eneo la Ngilu na kufunika barabara huku madaraja yakisombwa kwa baadhi ya maeneo yenye mito mikubwa katika tarafa ya Mawengi.

Wiki iliyopita tarafa ya mawengi yenye kata 3 ilikumbwa na majanga makubwa ya kusombwa madaraja mane yaliyokuwa kwenye mito mikubwa,, wakati mvua iliyonyesha wiki hii ikiacha madhara katika tarafa ya mwambao yenye kata za Lupingu,Lifuma,Lumbila,Makonde na Kilondo kwa kusomba mazao ,miundombinu ya mradi Wa maji pamoja na kufunika barabara kwa vifusi vikubwa vinavyoporomoka katika safu za milima ya Livingston

Wakizungumza kuhusu athari kiuchumi na kijamii za mvuo iliyonyesha usiku wa kuamkia marchi 2 wakati wakipambana kuokoa maisha ya wagonjwa waliyokwama kwasababu ya kukatika kwa mawasiliano ya barabara ,wakazi akiwemo Philip Fwalo, Meriana Kayombo ,Ibrahim Haule wanasema hadi sasa wanashindwa kusafirisha bidhaa kwenda sokoni na kuhatarisha maisha yao kwa kuendelea kutumia njia hiyo kwani hawana njia mbadala zaidi ya kutumia meli ambayo nayo haifanyi kazi.

"Kuna wavuvi wanahitaji mafuta kutoka mjini kwa ajili ya kuvulia samaki lakini mizigo hiyo haiwezi kufika ziwani kwasababu barabara haipitiki,Anasema Philip Fwalo mkazi wa Ludewa.

Kufuatia adha hiyo mbunge wa Ludewa Joseph Kamonga amelazimika kufika kushirikiana na TANROADS pamoja na wananchi kufungua barabara ili kurejesha tena mawasiliano ambayo yamepotea kwa zaidi ya siku nne kwasababu ya mmomonyoko wa ardhi uliyofunga barabara.

Kamonga amesema kuna ulazima wa kufungua barabara hiyo kwa kuwa ndiyo inatumika na kata zote za mwambao zenye wakazi zaidi ya elfu 20 hivyo inafaida kiusalama na kiuchumi kwa watu wa ukanda huo ambao uchumi wake ni wa ziwani na kilimo kiasi.

"Kata za mwambao zinategemea barabara ya Lupingu Ludewa kwa kila kitu kwa kuwa njia nyingine ambayo inaweza kuwatoa watu ukanda huo kuja Ludewa mjini ni kupitia meli ambayo nayo haifanyi kazi kwasasa,Anasema mbunge wa Ludewa Joseph Kamonga

Aidha mbunge huyo amesema hata ondoka katika eneo hilo hadi pale TANROADS watakapo maliza kazi kwasababu ni ngumu kukaa kwa amani bungeni wakati watu wake wanapata shida ya usafiri.

Nae katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Ludewa Amos Kusakula ambaye ameungana na mbunge kufanya zoezi la kuondoa kifusi kilichofunika barabara anasema jukumu la chama ni kuisimamia serikali hivyo sifanyike jitihada za haraka za kufungua maeneo yaliyofunikwa ili wananchi waendelee na majukumu yao ya kawaida.

"Nikiwa kama kiongozi wa chama tawala mwenye jukumu la kusimamia serikali ili kuwatumikia watu natoa rai kwa serikali ya wilaya ya Ludewa kuondoa changamoto hii ambayo sio salama kwa wananchi kiuchumuni na kijamii,Anasema Amos Kusakula katibu wa CCM wilayani humo. 

Kwa upande wake mkandarasi anaesafisha maeneo yaliyoathiriwa na mvua kubwa zinazonyesha wilayani Ludewa Frank Mayunga anasema wamefanya jitihada kubwa za kuondoa kifusi kwa maeneo kadhaa ili kuruhusu gari kupita 
huku pia akiomba kupewa siku mbili kurejesha barabara katika hali nzuri zaidi.

"Tanapambana sana kwa ushirikiano wa karibu na mbunge kufungua barabara na niwahakikishie wananchi nitamaliza jukumu hili baada ya siku mbili tu,Anasema Frank Mayunga mkandarasi.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post