Zoezi la anwani za makazi lamalizika hatua ya kwanza Kata tano za Jiji la Arusha

 Na Seif Mangwangi, Arusha

Wananchi wa Jiji la Arusha, wamepongeza hatua ya Serikali ya kutenga fedha kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli ya Utambuzi wa Anwani za Makazi na  majina ya mitaa.


Wakitoa maoni yao wakati wa kukamilisha siku ya mwisho ya utambuzi wa Anwani za Makazi na kuendelea na hatua nyingine baadhi ya wakazi wa Jiji la Arusha wamesema zoezi hilo litapunguza kero kwa wageni wanaokuja Arusha.


Ramadhani Juma, mkazi wa Kata ya Kaloleni,amesema Serikali inayoongozwa na Rais Samia inapaswa kupongezwa kwa kutenga fedha nyingi za kufanya kazi hiyo.


Amesema pia  zoezi hilo lina umuhimu mkubwa kwa wananchi kwa kuwa litarahisisha upatikanaji wa huduma za kijamii.


"Itasaidia watu kujulikana sehemu hali anayoishi ukiagiza bidhaa au ukipata tatizo mfano la nyumba kuungua moto inakuwa rahisi kusaidika hivyo zoezi hili ni muhimu kwa watu wote,"alisema mwananchi huyo.


 Alitoa rai kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa maofisa wa serikali na kuliunga mkono zoezi hilo kwa kuwa litasaidia maeneo yote kufahamika kwa uhalisia wake katika kanzi data ya serikali.


Mratibu wa zoezi hilo Kata ya Kaloleni, Ernesta Moshi, amesema zoezi hilo kwa kata hiyo limefanikiwa kwa asilimia 100 na wananchi wamelipokea kwa furaha kubwa.


Msimamizi huyo ambaye ni mmoja wa Maofisa Mipango wa Jiji la Arusha, amesema kadiri zoezi linapoendelea mwananchi wanafahamu na kuelewa umuhimu wake.


Amesema mwitikio ulikuwa mkubwa kwa kuwa walitoa elimu kwa wananchi kupitia vyombo vya habari na matangazo mbalimbali.


Kata ya Kaloleni ina mitaa mitatu ambayo ni Kaloleni Mashariki,Kaloleni Magharibi na mtaa wa mita 200 ambapo ni miongoni mwa kata Tano za Jiji la Arusha ambazo nyumba zake  zilishawekewa alama miaka kadha iliyopita.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post