KIJANA ALIYESHINDWA KUWNDELEA SEKONDARI KWA KUKOSA ADA AFIKIWA NA MRADI WA YAM

  

Kijana Andrew Mwakyoma wa pili kulia akiwa darasani akipata mafunzo ya ujasiliamali na wenzake 

KIJANA  Andrew Mwakyoma (17)  mkazi  wa Ibwanzi kata ya  Ihanu  wilaya ya  Mufindi mkoani Iringa  ameshindwa  kuendelea na masomo ya sekondari kidato cha tano kutokana na  mama yake  mzazi aliyekuwa akimsomesha kukosa sifa ya kuendelea kukopeshwa kwenye vikoba baada ya  kuwa na mkopo  sugu wa  Tsh 500,000.

Andrew ambae  alifaulu mtihani  wa  kidato  cha nne  mwaka 2020  kwa  kupata Divisheni 3 ya 24 ameendelea  kukaa nyumbani kwa zaidi ya mwaka  mmoja   sasa akilima vibarua  ili  kutafuta  fedha  .

Akizungumza jana  na  mwanadishi  wa  habari  hizi mara  baada ya mafunzo ya ujasiliamali kwa  vijana  wanaotoka kwenye mazingira  magumu  waliopo katika mradi  wa Youth Agency Mufindi (YAM)  kijana Andrew  alisema  kuwa  toka  alipoanza  elimu ya  sekondari  kidato cha kwanza  mahitaji ya  shule ikiwemo  ada aliyekuwa  akihusika ni mama  yake mzazi  ambae  alikuwa  akikopa fedha  hizo katika vikundi  vya  vikoba .

"Katika  familia  yetu  tupo  zaidi ya  watoto  na mimi  nina mdogo  zangu  watatu kwa  baba mmoja na hawa  wawili  baba  tofauti  na kati ya  hao mmoja  ameanza  sekondari  mwaka huu kidato cha kwanza na  mmoja yupo  shule ya msingi na  wawili bado kuanza  shule"


Hivyo  alisema  kutokana na uwezo mdogo  wa kiuchumi  wa  mama  yao amelazimika  kusubiri  kwenda  kidato cha tano ili  kupisha mdogo  wake  kwenda kuanza  elimu ya sekondari kidato  cha kwanza .

 " Bado  naendelea  kusubiri mama apate  fedha ili   niende  kuendelea na masomo yangu ya kidato  cha tano na nina tamani  sana  kwenda shule  ila sina  uwezo  wa  kipato na mama ndio  hivyo   tena hana  kitu kwa  sasa nafikiri  hata kwenda chuo cha maendeleo ya  jamii ili  nikapate  elimu ya  chuo hicho ila  sina fedha kiasi cha Tsh 800,000 za  kulipia "

Andrew  alisema   kwa  sasa amechukuliwa na mradi wa Youth Angecy  Mufindi (YAM) kama  kijana  anayetoka kwenye mazingira magumu na anaendelea na mafunzo ya  ujasiliamali  ili kufanya shughuli za ujasiliamali  kama  mtaji  kwake  kuendelea na  ndoto yake ya masomo .

Mama  mzazi  wa kijana huyo Joyce Mtovano  akizungumza kwa  njia ya simu na mwandishi  wa habari hizi  alisema  kuwa bado ana mpango  wa  kuwendeleza  kimasomo  kijana  huyo ila hana uwezo  wa  kifedha na hivyo anaomba  wasamaria  wema  kumsaidia   kijana  wake  kurudi  shule .

Joyce  alisema hadi  kijana  huyo amefanikiwa  kufika  kidato cha nne ni  kutokan  na  jitihada  zake  za kutafuta  fedha  kwa  njia ya kulima mashamba pia  kupika pombe  za  kienyeji .

Kuwa  hali yake ya  kiuchumi  si rafiki  kwani hata awali  alifanikiwa  kumsomesha  kijana   huyo  sekondari  kutokana na  kupika  pombe na  kuzungusha  fedha  kidogo  aliyoipata  kwa  kuweka kwenye  vikundi  vya   Vikoba  ambao  waliweza  kumpa mkopo  wa  Tsh  milioni 1.7  mkoapo  ambao hakuweza  kuulipa kwa  wakati   hivyo  kukosa  sifa ya  kuendelea  kukopa na hadi sasa ameendelea   kulipa mkopo  huo toka mwaka 2020  na bado anadaiwa  kiasi cha   shilingi 500,000.

Alisema  pindi atakapomaliza  mkopo  huo  ataweza  kuomba msamaha  kwenye  kikundi  ili  aweze  kurejea na  kuomba mkopo  tena utakaowezesha  kijana  wake  huyo  kuendelea na elimu ya chuo ama  sekondari.

Meneja  mradi  wa  YAM Zilipa Mgeni  alisema  lengo la mradi  wa YAM ni kuwapatia  elimu ya  ujasiliamali  vijana  waliopo  kwenye  mazingira magumu na  wale  walioacha  shule  ya  msingi kama  watoto  hao  wanarejeshwa  shule  kuendelea na masomo .

"Mradi  wetu  ni wa  miaka minne umeanza  mwaka jana unafadhiliwa na  taasisi ya  Deacones  chini ya serikali ya   Finiland  na unatekelezwa na taasisi ya Foxes Community and  Wildlife Trust  kwa  kushirikiana na Halmashauri ya  wilaya ya  Mufindi na  unatekelezwa  kwenye  vijiji  16  vya kata  tatu  za Ihanu, Mdabulo na Luhunga wilaya ya Mufindi na  vijana 770  na  watoto  ndio watakaonufaika na maradi  huu "

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post