Hatimaye Shule ya Msingi Mkonoo yapata maji safi

Arusha

Na Mwandishi Wetu

Shule ya Msingi Mkonoo iliyopo katika halmashauri ya Jiji la Arusha leo imepokea mradi wa maji safi na salama pamoja na vifaa vya michezo kutoka kwa msamaria mwema  Hosiana Mollel mzaliwa wa eneo hilo na aliyepata elimu yake ya msingi shuleni hapo.


Akimkabidhi mradi huo wa matanki mawili ya maji yenye ujazo wa lita elfu ishirini uliogharimu zaidi ya shilingi milioni kumi kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Dkt John Pima amesema ameshukuru kuona nia yake ya kuisaidia shule hiyo na jamii ya Mkonoo inatimia.


Mara baada ya kupokea mradi huo Dkt Pima amesema “Huu ni mfano wa kuigwa, kuona mtu anakumbuka kwao huu ni uzalendo mkubwa sana ambao kila mwenye uwezo wa kufanya kama huyu dada ni muhimu kufanya hivyo, kwani licha ya kusaidia wananfunzi na wakazi wa Mkonoo lakini pia ameisaidia serikali, kikubwa niwaombe walimu na wanafunzi kutunza mradi huu ili utumike kwa muda mrefu” Alisema Dkt Pima.


Akizungumza na wanafunzi na walimu wa shule hiyo, Dkt Pima aliwaambia ofisi yake ina mpango wa kufanya maboresho makubwa kwenye shule hiyo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa madarasa mapya ya ghorofa kama ambavyo Rais Samia Suluhu Hassan amelitaka jiji la Arusha kujenga majengo ya ghorofa katika shule.


“Nimeambiwa na pia nimeona hapa kunahitajika ukarabati wa majengo, sasa naomba niwahakikishie kuwa nitafanya ukarabati mkubwa na pia nitajenga majengo mapya ya madarasa tena ya ghorofa kwani hata Rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassan anataka tujenge majengo ya shule ya ghorofa, kwa hiyo naomba niwatoe hofu kuhusu hilo” Alisema Dkt Pima.

Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dkt John Pima (kushoto) na Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Mkonoo Loshiani Manimo (kulia)


Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Lushiani Manimo amesema awali kulikuwa na uhaba wa maji shuleni hapo jambo ambalo lilipelekea utoro kwa baadhi ya wanafunzi na kwamba kwa sasa mahudhurio yameanza kuwa mazuri hivyo anategemea ufaulu kuongezeka.


Akizungumza mara baada ya kugawa vifaa vya michezo kwa wanafunzi hao, Hosiana Mollel amesema sababu kubwa iliyopekea hadi kutafuta wafadhili kwa ajili ya mradi huo inatokana na changamoto kubwa ya maji aliyoipitia wakati akisoma katika shule hiyo.


“Maji yalikuwa changamoto sana hapa, na ikizingatiwa kuwa eneo hili lina ukame, wanafunzi tulipata shida sana, ndiyo maana nikaamua kutafuta wahisani ambao leo hii wamenisadia kwa kiasi kikubwa na sasa nina furaha kuona shule yangu imepata maji, na ninaahidi kuwa sitaishia hapa, pale ambapo nitaweza kusaidia nitaendelea kusaidia” Alisema Hosiana.

Matanki ya maji yenye ujazo wa Lita elfu ishirini yaliyotolewa na msamaria mwema Hosiana Mollel kwa shule ya Msingi Mkonoo iliyopo Jiji la Arusha.

1 Comments

This is received, thanks for your comments, will come back to you

  1. Goyang Hotel and Casino - Cherokee, NC - Goyang
    Experience our lively, 깡가입코드 upscale casino resort near the North 에이스 포커 Carolina border. It's home to 총판 the ultimate in entertainment, 슬롯추천 dining, hotel 가상 화폐 추천 and more.

    ReplyDelete
Previous Post Next Post