Rc Mjema awataka Tarura na TANROADS kutatua kero za wananchi

 Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema amewaagiza wasimamizi ukarabati na ujenzi wa barabara mjini TANROADS pamoja na wasimamizi ukarabati na ujenzi wa barabara vijijini TARURA kusimamia sheria za barabarani ili kuondoa kero na migogoro kwa wananchi.


Ameyasema hayo leo kwenye kikao cha bodi ya barabara mkoa wa Shinyanga kilichohudhuriwa na viongozi wa serikali pamoja na wadau wengine ambapo mkuu huyo wa Mkoa amesema ni wajibu wa kila mwananchi kutunza miundombinu ya barabara.


Amezitaja baadhi ya changamoto zinazoleta matokeo hasi kwenye miundombinu ya Barabara ambapo amesema katika changamoto hizo ni pamoja na  tabia ya wananchi kujimilikisha miundombinu ya Barabara, kufanya shughuli za kilimo kwenye  kando kando ya Barabara pamoja  na kufanya biashara kwenye hifadhi ya Barabara ambapo amewaagiza viongozi miundombinu ya Barabara inaendelea kuwa salama.


Mjema amewaelekeza wasimamizi, ukarabati na ujenzi wa Barabara TANROADS pamoja na TARURA mkoa wa Shinyanga kuhakikisha wanaweka taratibu za kufanya matengenezo ya dharura kwa maeneo yenye changamoto yanayosababisha kutopitika hasa katika kipindi cha mvua.


“Ninawaagiza wasimamizi wakala wa Barabara ndani ya TANROADS na wakala wa Barabara ndani ya TARURA kusimamia sheria katika utendaji kazi wa majukumu yenu meneja atakayefanya uzembe nakutokutimiza wajibu wake tutaongea vizuri Barabara hizi lazima ziangaliwe”.


Mkuu huyo wa mkoa wa Shinyanga Mjema amesema changamoto nyingine ni magari kubeba  uzito wa kiwango kilichowekwa huku akisisitiza  kuwekwa kwa alama za Barabarani pamoja na kufanyiwa marekebisho taa ambazo hazifanyikazi ili kuondoa changamoto kwa wananchi. 


Mheshimiwa Mjema amewataka viongozi ngazi ya chini kuhakikisha wanasimamia suala la usafi kwenye miundombinu ya Barabara ambapo amesema wapo wananchi wanaotupa taka kwenye mitaro ya Barabara hali ambayo inasababisha mmomonyoko kwenye Barabara.


Aidha Mjema amesema licha ya  changamoto mbalimbali zilizopo pamoja na ufinyu wa bajeti ametoa pongezi kwa wakala wa wa Barabara mijini TANROADS pamoja na wakala wa Barabara vijijini TARURA kwa kuendelea kusimamia vizuri miundombinu ya Barabara na kuhakikisha Barabara zote zinapitika.


Kupitia kikao hicho mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amehoji kuhusu utekelezaji wa daraja lilipo Kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga ambapo pia ameshauri kupewa kipaumbele wakandarasi wa Mkoa wa Shinyanga.


“Tutumie wakandarasi waliopo kwenye mkoa wetu wa Shinyanga kwa sababu kuna baadhi ya Barabara hapa Manispaa mkandarasi aliyekuwa anatakiwa kuripoti kufanya ile kazi imemchukua miezi mitatu au minne haonekani kwahiyo tuendelee kusisitiza kupitia kikao hiki kwamba waendelee kuchukua na kutumia wakandarasi waliopo kwenye mkoa wetu ili kuendelee sisi wenyewe kuwabana lakini lingine nila daraja la kata ya Ndala hii ilikuwa ni ahadi ya mheshimiwa Rais itekelezwe kama ilivyoelekezwa”.


Kwa upande wake meneja msimamizi ukarabati na ujenzi wa barabara vijijini TARURA Enjinia Oscal Gilbert amesema ujenzi wa daraja lilipo kata ya Ndala unategemea bajeti ya mwaka huu wa fedha 2022-2023 ili kuondoa changanamoto kwa watuamiaji.


Enjinia Gilbert amesema wataendeleo kuwapa kipaumbele wakazi wa mkoa wa Shinynga katika shughuli mbalimbli kwa kufuata sheria ya Barabara.


Kwa upande wake mbunge wa jimbo la  Kishapu Boniphace Butondo amewapongeza wakala wa wa Barabara mijini TANROADS pamoja na wakala wa Barabara vijijini TARURA kwa kuendelea kusimamia na kutekeleza vizuri miradi mbalimbali ya  miundombinu ya Barabara huku akiwaomba kuongeza jitihada katika utekelezaji wao wa miradi ili kupunguza changamoto kwa wananchi.


Naye meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko amewashauri wakala wa Barabara kuweka  kipaumbele cha kuchimba mitaro inayopitisha maji ili kulinda Barabara zisiharibike mapema na kusababisha athari kwa wananchi hasa katika kipindi cha masika.


“Barabara nyingi zimekuwa haziwekewi mitaro ya kutosha kuondoa maji kwenye kingo zake za Barabara sababu hii inasababisha Barabara nyingi kuharibika mapema sana mimi nishauri hasa kwa TATURA kwanza mitaro ingekuwa ni muhimu zaidi kuliko Barabara mitaro ikishakuwa imara zaidi itakuwa inaokoa Barabara zitakapokuwa zinatengenezwa”.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post