MTOTO WA MIAKA 10 AUZIWA ARDHI GOBA, HAKIMU AMPA TUZO

Na Mwandishi Wetu, Pwani


MWENYEKITI wa Baraza la Ardhi na Nyumba Wilaya ya Kinondoni lililopo Mwananyamala  Jijini Dar Es Salaam Longinus Rugarabamu amempatia tuzo mtoto Lulu Victor Kayombo Mkazi wa Mbezi Beach, Hakimu huyo amempa tuzo hiyo Lulu Kayombo kumiliki shamba lenye ekari 7 lililopo Matosa kata ya Goba  ambalo alilinunia akiwa na miaka 10 baada ya awali kutoa Tuzo nyingine kwa mdaiwa kwa kesi hiyo hiyo na kusababisha sintofahamu kubwa

     

Longinus anadaiwa kutoa hukumu mbili ndani ya muda mfupi na kuwapa ushindi wadai na wadaiwa kwa nyakati tofauti ambapo awali Lulu Kayombo alishindwa kuthibitisha manunuzi na kutoa vielelezo vilivyoonesha alinunua shamba hilo lenye ukubwa wa ekari (7) mwaka 2006 akiwa na umri wa miaka 10 shamba lililopo eneo la Matosa kata ya Goba


Ilielezwa mahakamani hapo kwamba eneo hilo la ardhi linamilikiwa kihalali na Lulu Victor Kayombo na tayari limepimwa na kuwa na viwanja namba 200, 201, 202, 203, 204, 205, 206, 207, 208, 209, 210, 211, 212, 2013 na 214 Kitalu F Mtaa wa Matosa Tegeta Manispaa ya Kinondoni


Wakizungumzia sakata hilo Mohamedi Rajabu amesema inashangaza kuona Baraza  hilo hilo ambalo lilishatoa hukumu katika shauri hilo hilo namba 454 la mwaka 2015 na mwenyekiti wa baraza huyo huyu kuwapa ushindi huku 

akinukuu vifungu mbalimbali vya sheria kwamba mtoto wa miaka 10 hawezi kuwa mnunuzi halali lakini Leo mwenyekiti yule yule anatoa ushindi kwa mtoto huyo kuwa mnunuzi halali


Akizungumza baada ya ushindinm kutolewa kwa hukumu  hiyo, Mariam Hussein ambaye ni mke wa marehemu Rajabu Hemedi Litumbui aliyefariki 24.05.2006 amesema eneo bishaniwa ni Mali ya familia na wakati mume wake anafariki mnunuzi (Lulu) alikuwa ana umri wa miaka 10 tu.


Ameshangaa na kuuliza mtoto huyo aliwezaje kunununua eneo hilo  wakati hata msimamizi wa mirathi alikuwa hajateuliwa? Je sheria za nchi zinaruhusu mtoto kufanya manunuzi akiwa chini ya miaka 18? Alihoji


Ameongeza kuwa, iweje kuwe na hukumu mbili ndani ya muda mfupi na Mwenyekiti huyo huyo ambaye alishatoa hukumu na kuandika utekelezaji ufanyike, amehoji  "kwanini Mwenyekiti wa baraza asifike katika eneo husika ili kujiridhisha kwa kuangalia uhalisia wa eneo tajwa na badala yake tumenyang'anywa haki yetu bila kufuta sheria za nchi "Naomba serikali ichunguze suala hili hususani TAKUKURU kwani kuna dalili za rushwa ya waziwazi katika shauri letu", alisema 


Akijibu tuhuma hizo kwa njia ya simu Mwenyekiti huyo wa Baraza la Ardhi na nyumba Jaji, Rugarabamu amekiri kuwepo kwa mapungufu katika shauri hilo  kutokana na wanasheria wa pande zote mbili kutomkumbusha kama kulikuwa na hukumu nyingine ya awali ambayo ilishatoka 

"Ndugu mwandishi Mimi nipo likizo mpaka tarehe 10/01/2022 hivyo sitakuwa ofisini, ninashauri walalamikaji waende Mahakama kuu kukata rufaa kupinga hukumu ya pili kama kuna ulazima wa kufanya hivyo, lakini kwa mamlaka ya mabaraza hatuna uwezo wa kubadili chochote


Kwa upande wake wakili Bensoni Kuboja  amesema, anashangaa kwanini hukumu tajwa haikutaja mawakili kushiriki katika shauri hilo wakati mawakili wote walishiriki katika shauri hilo tangu mwaka 2015, "naomba chunguza kurasa zote uone sehemu gani mawakili wametajwa?


Awali inasemekana Lulu Kayombo aliwasilisha kesi mahakamani akidai eneo lake kuvamiwa na Mariam Hussein na Mohamedi Rajabu, na katika utetezi walitakiwa kupeleka ushahidi/vielelezo ndo ikabainika kutokuwepo na mkataba halali wa mauziano pamoja na mapungufu ya mnunuzi kuwa alikuwa na miaka 10 maana amezaliwa mwaka 1996 na mauziano ni mwaka 2006

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post