Na Mwandishi Wetu, Arusha
Wananchi wa Kijiji cha Mareu, Kata ya King'ori Halmashauri ya Wilaya ya Meru wameishukuru Serikali ya awamu ya sita ikiongozwa na Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa Shilingi Milioni 250 fedha za tozo za miamala ya simu kwaajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya katika Kijiji hicho.
"Tunamshukuru Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kutoa fedha hizi kwani tulikuwa tunafuata huduma za afya Mkoa wa jirani au katika Hospitali ya Wilaya iliyopo mbali na kijiji hichi, hivyo niwaombe Watanzania wenzangu tushirikiane katika Kujiletea maendeleo" amesema Janeth
Kwa upande wake Magdalena amesema Wanawake wa Kata ya King'ori hawana budi kumshukuru Rais kwa ujenzi wa Kituo hicho cha Afya kwani ni wanufaika wakuu hususani katika Suala la kujifungua.
"Tunaishukuru Serikali kupitia fedha za tozo tutajifungulia Sehemu salama na kupata huduma Bora za afya.
Katika ziara hiyo Naibu Waziri, Dkt. Godwin Mollel aliongozana na Dkt.John D Pallangyo Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki ikiwa ni ziara ya Mhe.Mbunge kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo Jimboni sambamba na kusikiliza na kutatua kero za Wananchi.