Jenista awafunda watumishi wa wizara yake

 Na Doreen Aloyce,Dodoma


WAZIRI Ofisi ya waziri mkuu sera,Vijana,ajira na wenye ulemavu Jenista Mhagama amewataka watumishi wa Wizara hiyo kuendelea kusimamia Majukumu yao kwa ufanisi kwa kila idara kutekeleza  Programu  walizonazo  pamoja na kutumia maarifa kuleta mafanikio katika wizara hiyo.


Kauli hiyo ameitoa leo Jijini Dodoma wakati alipokuwa kwenye kikao na wafanyakazi wa Ofsi hiyo pamoja na Taasisi zake waliopo Dodoma kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali yakiwemo mafanikio yaliyojitokeza Katika kipindi Cha mwaka 2021.


Aidha Mhagama amesema kuwa Katika kufanikisha kusudi la Serikali  wafanyakazi hao wanapaswa  kudumisha mshikamano ,uwajibikaji wa pamoja katika kutekeleza Majukumu ,uaminifu huku wakitumia hekima na busara kwenye utendaji kazi wao.


"Pia niwatake kuendelea Kupambana  na Rushwa na vitendo ambavyo haviendani na utumishi wa umma badala yake mtumie busara ,hekima Katika ufanisi wa kazi huku mkiwa wawazi kutafuta haki zenu kusiko Kuwa na malalamishi ambayo hayana tija "amesema Jenesta.


Amesema kuwa Wizara imeweza kufanikiwa mambo mbalimbali ikiwemo ujenzi wa vyuo sita vya watu wenye ulemevu ambavyo vitasaidia  kuweza kuboresha ujuzi na kuboresha maisha yao ya Kila siku huku Serikali ikitenga Bilioni Tisa kwa ajili ya ujenzi wa jengo la msajili wa vyama vya siasa.


"Pia tumeKupokea fedha Bilioni 2.5 kwa ajili ya ujenzi wa Tume ya usuluhishi na usimamizi, kituo chenye sura ya kimataifa ni niwatake  mtakaosimamia  ujenzi huo kuwa makini ili jengo liwe imara na Hali ya juu ."


"Na tumepokea Bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa Kiwanda Cha kipya Cha kisasa Cha kupiga chapa ambacho kitakidhi vigezo na kusaidia Serikali kufanya kazi kwa Viwango vya juu" amesema Mhagama.


 Kwa upande wake Katibu wa Wizara hiyo Tixon Nzunda amesema kuwa kutokana na maelekezo ya waziri kupitia Ofsi yake watayafanyia kazi huku akiwataka watumishi kuonyesha Umoja na mshikamano ili waweze kutimiza malengo yao.


"Tumefaanya maboresho mbalimbali Sekta ya hifadhi za Jamii na uwekeji wa mifumo ambayo itarahisha wanachama kupata huduma Kwa urahisi bila ubaguzi wowote kwani wote ni Ofsi moja"amesema Tixon.


Awali wakitoa kero zao mbele ya waziri Mhagama wajumbe wa kikao hicho wamesema Serikali kupitia Ofsi yake wanapaswa kuendelea kuboresha maslahi ya watumishi na kuweka mazingira rafiki ya kutatua changamoto zao.


Pia wameomba kuwepo mafunzo maalumu ya kuwaandaa watumishi kabla ya kustaafu ambayo yatawasaidia kukabiliana na maisha wanapo staafu kwani Wengi wao huwa wanakumbana na changamoto wanapomaliza muda wao wa kazi kwa kukosa elimu hiyo.


Hata hivyo wameiomba Serikali kupitia Ofsi ya waziri mkuu  kushughulikia walemavu wapatiwe viwanja kwa riba nafuu kwa ajili ya kuweka Makazi yao  ambayo wataweza kulipa taratibu.


Mwisho

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post