JAMHURI YAFUNGA USHAHIDI KESI YA BABU WAWILI WALIOBAKA MJUKUU KWA ZAMU.

 


Na Serengeti Media Serengeti Media Centre


SERENGETI.Kesi inayowakabili Babu wawili wanaoshitakiwa kwa kosa la kubaka mjukuu wao wa miaka (12) kwa  zamu imeendelea kuunguruma kwa mashahidi wawili wa Jamhuri akiwemo daktari aliyefanya uchunguzi na mpelelezi katika mahakama ya wilaya ya Serengeti.


Washitakiwa ni Hamisi Maganga(50)na Magembe Magangila(50) wote wakazi wa Natta ambao kwa pamoja walikamatwa desemba 17,2021 kwa tuhuma za kumbaka mtoto huyo kwa zamu na kumuumiza hali iliyopelekea kulazwa katika Kituo cha Afya cha Natta kwa matibabu.


Katika kesi ya Jinai namba 1/2022 mbele ya Hakimu Mkazi wa Wilaya Adelina Mzalifu daktari Daktari Juma Kipingu akiongozwa na Mwendesha Mashitaka wa Jamhuri Paschael Nkenyenge ameiambia Mahakama kuwa alimpokea mtoto huyo akiwa ameumizwa sana sehemu za siri kutokana na kuingiliwa na kumhudumia kwa kumshona na kumwongezea damu unit 2 na shahidi wa pili aliyewasilisha maelezo yake ni askari wa upelelezi.


Kesi hiyo imehairishwa hadi Februari8.2022 ambapo shahidi wa mwisho wa Jamhuri atahitimisha maelezo yake,washitakiwa wamerudishwa mahabusu hadi tarehe hiyo.This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post