BINTI AMUUA MAMA YAKE MZAZI ILI ARITHI MALI, MWILI WAGUNDULIWA BAADA YA MWAKA MMOJA

Na Mwandishi Wetu, Moshi

*• Meya Juma Raibu ashindwa kujizua amwaga machozi na kulaani vikali*

*•Meya Raibu alipongeza Jeshi la Polisi, Awaasa vijana kuacha Tamaa na starehe*


Ikiwa zimepita siku kadhaa toka litokee tukio la kijana mmoja jijini Arusha kumuua mama yake mzazi Kwa tamaa ya Mali, Limegundulika tukio lingine la kinyama mkoani Kilimanjaro katika Manispaa ya Moshi ambapo binti mmoja aliejulikana Kwa jina Moja la Wendy amemuua Mama yake mzazi (Mama Ipepu) ambae ni Nesi mstaafu wa Hospital ya KCMC.


Jeshi la Polisi limeufukua Mwili huo leo tarehe 09-01-2022 katika kata ya Rau baada ya kumhoji binti huyo Kwa zaidi ya wiki mbili sasa Kisha kukiri kumchinja mama yake Kwa panga na kumfukia nyumbani hapo.


Ni takribani Mwaka sasa ndugu na majirani walipokuwa wamuulizia mama huyo walipatiwa majibu na binti huyo kuwa amesafiri Kwa matibabu nje ya nchi.

 

Akizingumza Kwa uchungu huku akilengwalengwa na machozi Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Ndg Juma Raibu ameonesha kusikitishwa na kitendo hicho na amelaani vikali tabia ya vijana kuendekeza tamaa na kukosa uvumilivu wa utafutaji Mali Kisha wanaishia kufanya matendo ya kinyama.

"Kiukweli hili ni tukio la kutisha, nitoe pole Kwa familia ndugu na majirani wote mliofika hapa, nimepata huzuni sana kuona jinsi gani ya taamaa Mali imetufikisha hapa, nalaani na ninatoa wito Kwa vijana wenzangu wote nchini kuacha kupaparikia Mali na starehe mwisho wake tunageuka kuwa wanyama kiasi hiki, yaani unamuua mama mzazi?,"alihoji na kuongeza...

 "Hivi unakuwa huogopi laana na adhabu ya mola? nalipongeza Jeshi letu la Polisi Kwa hatua hii nawatia Moyo mwendelee na kazi hii njema ya kufichua na kudhibiti wahalifu wa namna hii na wanaoshirikiana nao" amesema

Tayari madaktari wameanza kufanyia uchunguzi wa postmortem Mwili huo kwajili ya hatua zinazofuata.


2 Comments

This is received, thanks for your comments, will come back to you

  1. Thanks kwa habari moto moto... Na Seif amekuwa mstari wa mbele kututumia news everyday. Na tunakuwa update often.

    ReplyDelete
  2. Ahsante kwa habari zinatufikia kwa wakati,keep it up Seif

    ReplyDelete
Previous Post Next Post