Rais Samia uso kwa uso na wakuu wa sekondari 5,000

Rais Samia Suluhu Hassan

 

Na Mwandishi Wetu


RAIS  Samia Suluhu Hassan kesho (Jumatano),  anatarajiwa kufungua mkutano wa wakuu wa shule za sekondari Tanzania.

Mkutano huo wa siku tatu unataratibiwa na Kampuni ya Global Education Link (GEL).


Katibu Mkuu wa Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari (TAHOSSA), Titus Jumanne alisema mkutano huo utakaofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City unatarajiwa kuhudhuriwa na walimu 5,000 nchi nzima.


 Alisema mkutano huo wa 16 unawaleta pamoja wakuu hao wa shule ili kubadilishana mawazo, uzoefu, changamoto, mafanikio na utekelezaji wa sera na mipango inayotolewa na serikali.


Alisema kwenye mkutano huo kutakuwa na tukio la utoaji wa zawadi mbalimbali kwa shule, walimu na wanafunzi waliofanya vizuri kitaaluma.


Alisema mkutano huo utajadili mafanikio mbalimbali ya elimu yaliyopatikana katika awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ikiwemo ujenzi wa shule na maelfu ya madarasa mapya.


Aliishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kutenga fedha kwaajili ya ujenzi wa shule moja ya wasichana kwa mikoa 10 hali ambayo alisema itasaidia kuwapunguzia adha ya kusafiri umbali mrefu watoto wa kike kwenda shule.


Alisema awamu ya sita imejitahidi kuhakikisha ufaulu kwenye elimu ya msingi na sekondari unaongezeka kwa kuweka miundombinu na walimu wa kutosha yote hayo ikiwa ni kuboresha elimu.


“Hiki ni kipindi cha kushangilia mafanikio ya elimu katika kuadhimisha miaka 60 ya Uhuru Rais wetu Samia atakutana na wakuu wa shule nchi nzima na kuzungumza nao masuala mbalimbali yanayohusu elimu na kuwapa mwelekeo wake kwenye sekta hiyo,” alisema Jumanne.


“Mkutano huu itakuwa fursa kubwa kwa walimu wakuu wa shule za sekondari kukaa pamoja na kubadilishana mawazo na uzoefu wa namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali lengo ikiwa ni kuifanya sekta ya elimu iendelee kufanya vizuri,” alisema Jumanne.


Alimshukuru Rais Samia kwa kupeleka Sh bilioni 100 kwaajili ya ujenzi wa shule za sekondari mpya zipatazo 214 ambazo zitajengwa kwenye majimbo yote nchini ambapo Rais pia aliagiza Sh bilioni 30 zitumikekujenga shule mpya za wasichana pekee ambapo kwenye mikoa 10 itajengwa shule moja moja ya wasichana.


“Pia Serikali ya awamu ya sita ya Rais Samia imeagiza ujenzi wa shule za nsekondari 1,000 zitakazojengwa katika kata ambazo hazina shule za sekondari hii haijapata kutokea na serikali ya awamu ya sita inastahili pongezi za dhati kabisa,” alisema Jumanne


Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo alithibitisha kuwa Rais Samia atakuwa mgeni rasmi kwenye mkutano huo wa walimu wa nchi nzima.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post