Mama amuunguza moto mtoto wake akishirikiana na binti yake kwa madai ya kuiba flash

ACP George Kyando

 Na Mapuli Misalaba, Shinyanga


Watu wawili wa familia moja Mama na Binti yake ambao ni wakazi wa mtaa wa Dome kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kumchoma moto mtoto wao wakimtuhumu kuiba Flash-Disc (flash mweko).


Imedaiwa kuwa wanawake hao Adelida Leonard mwenye umri wa miaka 50 na binti yake Beatrice Mwombeki mwenye umri wa miaka 28 wamemuunguza mtoto huyo sehemu mbalimbali za mwili wake kwa kutumia mkasi wa kukatia fensi uliochemshwa kwenye jiko la mkaa hali iliyomsababishia majeraha makubwa.


Watu walioshuhudia tukio hilo wameiomba Serikali na Mamlaka zake kuendelea kuielimisha jamii kuhusu madhara ya ukatili wa kijinsia hasa kwa Watoto ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote wanaoendelea kujihusisha na vitendo hivyo.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Dome Solomoni Nalinga ametumia nafasi hiyo kuikumbusha jamii kuwa makini na kuepuka kutoa adhabu zinazosababisha madhara kwa watoto na watu wengine.


“Wazazi wawe wavumilivu wasiwe wanajichukulia sheria mkononi kwa sababu sisi viongozi tupo wanapokuwa wanaona kuna jambo limewashinda tunaweza tukazungumza hatua moja baada ya nyingine kwa sababu kuna taasisi zinazo husika na mambo ya watoto na wawazoeshe watoto kwenda kwenye nyumba za ibada” 


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando amethibitisha kutokea kwa tukio hilo amesema watuhumiwa ambao ni Adelida Leonard (bibi) na Beatrice Mwombeki (mama mzazi) wamekamatwa na madhura amelazwa katika hospital ya rufaa mkoa wa Shinyanga.


Tukio hilo linatokea wakati  tanzania  na mataifa mengine duniani yakiadhimisha siku 16 za kupinga ukatili na unyanyasaji wa kijinsia

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post