Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro yaotesha Miti 8000

 Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro

Katika kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi, Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro imeshiriki katika zoezi maalum endelevu kwa  kuotesha miti 8,000 katika maeneo ya Samanga na Singa wilayani Rombo, mkoani Kilimanjaro.


Awali maeneo hayo  yalikuwa yameathiriwa na mimea vamizi jamii ya Miwato (Acacia Mearnsii) ambapo Hifadhi iliondoa mimea hiyo mwaka jana wa fedha. 


Kwa mujibu wa Meneja Mawasiliano wa hifadhi za Taifa (TANAPA),Kamishna Msaidizi Paschal Shelutete, mgeni Rasmi katika shughuli hii alikuwa Balozi wa Utalii wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Sharon Ringo ambaye katika salamu zake amewataka wakazi wanaozunguka Mlima huo kutunza miti hiyo.

Wadau wengine walioshiriki ni wananchi wa Kijiji cha Samanga, wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka, Maafisa wa Halmashauri ya Wilaya- Rombo na Maafisa kutoka Sekretariet ya Mkoa wa Kilimanjaro.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post