CRDB Super cup yamalizika Arusha kwa Tanzanite Queen kuibuka kidedea

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela  akimkabidhi Nahodha wa timu ya Simu banking   kombe mara baada ya kushika nafasi ya Kwanza  katika fainali za CRDB super cup

 


Na Woinde shizza , Arusha


Timu ya mpira wa Pete ya Tanzanite queen   pamoja na timu ya mpira wa miguu ya  simu banking imeweza kuibuka kidedea na kunyakua kitita ela pamoja na makombe katika mashindano ya  CRDB super cup.


Akizungumzia mashindano hayo mkurugenzi  wa rasilimali watu  kutoka benki ya CRDB  Siaopharo Kishimbo alisema kuwa mashindano hayo yalianza kutimua vumbi mapema mwezi September mwaka huu ambapo mashindano hayo yalishirikisha  timu kutoka katika  matawi yote ya benki hiyo Tanzania nzima.

"Tulishirikisha timu zote katika matawi baada ya apo zikachujwa hadi zikabaki timu za kanda na makao makuu ambapo jumla zilikuwa 16 Kwa mpira wa miguu pamoja na timu nane za mpira wa Pete"alisema Kishimbo 

Alitaja timu zilizoibuka kidedea Kwa upande wa mpira wa miguu timu ya Simu banking ilifanikiwa kushika nafasi ya Kwanza ambapo ilifanikiwa kuondoka na kitita cha shilingi milioni tano ,medali pamoja na kombe huku nafasi ya pili ikishikiliwa na timu ya makao makuu ya crdb(HQ)ambapo iliondoka na kitita cha shilingi milioni tatu  ,kombe na medali huku nafasi ya tatu ikishikiliwa na timu ya Nia Fc ambayo ilifanikiwa kuondoka na kitita cha shilingi milioni moja.

Kwa upande wa mpira wa Pete timu ya Tanzanite queen  iliibuka kidedea na kufanikiwa kuondoka na kitita cha shilingi milioni tatu ,kombe na medali huku nafasi ya pili ikishikiliwa na timu ya ulipo tupo ambayo iliondoka na kitita cha shilingi milioni mbili ,medali na kombe huku nafasi ya tatu ikishikiliwa  hodari Queen ambayo ilifanikiwa kuondoka na kitita cha shilingi milioni moja  kombe pamoja na medali.


Akizungumzia mashindano hayo mara baada ya kukabidhi makombe 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema kuwa nia yakuandaa mashindano hayo ni kuwaletea pamoja wafanyakazi wa benki hiyo na kibadilishana uzoefu na ujuzi pamoja  na kuhamasishana kufanya mazoezi

Alisema kuwa hii ni mara ya Kwanza mashindano hayo kufanyika na hayataishia hapa bali yatakuwa yanafanyika Kila mwaka .

Aliwasihi wafanyakazi wa benki hiyo kuendelea kufanya michezo na mazoezi kwani michezo inasaidia kujenga ushirikiano mzuri pamoja na kuendelea kutengeneza afya  .


Alisema kuwa  zipo changamoto mbalimbali ambazo wamekutana nazo katika mashindano haya ikiwemo ya uhaba wa viwanja vya kufanyika mazoezi Kwa timu zao  na kubainisha kuwa  katika michezo ijayo wataangalia namna ya kuzitatua mapema.Timu ya mpira wa Pete ya Tanzanite queen wakiwa katika  picha ya pamoja   mara baada ya kukabidhi kombe fedha taslimu kiasi Cha shilingi milioni tatu


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post