Waziri Ummy: Tegemeeni makubwa ujenzi wa barabara za vijijini

 

Na. Angela Msimbira Mwanga


Waziri wa Nchi  Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Ummy Mwalimu amesema dhamira ya dhati ya Serikali  ya awamu ya sita ni kuhakikisha inajenga miundombinu ya barabara maeneo ya vijijini kwa kuongeza bajeti ya ujenzi wa barabara maeneo ya vijijini kupitia wakala wa barabara Mijini na Vijijini (TARURA)


Akikagua  ujenzi wa  barabara  ya Kisangara - Shighatini na kifula - Butu katika Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Leo Waziri Ummy amesema bajeti ya  Tarura katika Halmashauri hiyo imeongezeka kutoka shilingi milioni 695 kwa mwaka wa fedha 2020 hadi kufikia shilingi bilioni 3.5 kwa mwaka wa fedha 2021


Amesema kuwa wananchi wategemee mabadiliko makubwa katika suala zima la ujenzi wa miundombinu kwenye maeneo ya vijijini lengo likiwa ni kuwapunguzia adha wananchi na kufungua uchumi wa wakazi wa Mwaga kwa kuwa barabara nyingi zitafunguliwa, 


Amemuagiza   Mkandarasi anayejenga barabara hiyo Elerai Construction Co Limited kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa  barabara hizo kwa wakati kwa kuhakikisha wanafuata  viwango vilivyowekwa na Serikali


Aidha, ujenzi wa barabara ya Kisangara - Shighatini (km3. 57) na Kifula - Butu (km 3.57) itajengwa kwa kiwango cha lami na itagharimu zaidi ya shilingi  milioni  441.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post