WAFANYABIASHARA WA MBAO WAKIMBIA NJOMBE KWA MADAI YA KUPANDISHIWA USHURU

 NA MWANDISHI WETU, NJOMBE


Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Njombe limedai kukabiliwa na wimbi la kukimbiwa na wafanyabiashara wa mbao kutokana na Halmashauri hiyo kudaiwa kutoza kiwango kikubwa cha ushuru kuliko halmashauri nyingine.

Halmashauri ya Wilaya ya Njombe inatoza ushuru wa Tsh 200 kwa kila ubao jambo ambalo linasababisha wafanyabiashara wengi kukimbilia Halmashauri ya Wilaya ya Makete na Mufindi Iringa zinazotoza chini ya kiwango hicho.

Halmashauri ya wilaya ya Njombe ina zaidi ya mwaka mmoja sasa tangu ipitishe kiwango kipya cha tozo kwa kila ubao lengo likiwa ni kuongeza kiwango cha makusanyo jambo ambalo limekuwa na matokeo tofauti kwa wafanyabiashara na wakulima wa miti.

Javan Ngumbuke ambaye ni diwani wa kata ya Ukarawa ne Getruda Chungwa ambaye ni diwani wa viti maalumu wanasema halmashauri hiyo imeanza kuathirika kiuchumi kwasababu inakimbiwa kila kukicha na wafanyabiashara kutokana na kiwango kikubwa cha ushru wa ubao hivyo jitihada za haraka za kupunguza tozo hizo zinatakiwa kuchukuliwa ili kuokoa uchumi wa misitu na mbao.

"Tutakiwa kufanya maamuzi kupitia kikao hiki cha baraza juu ya tozo kubwa za mbao kwasababu wafanyabisahara wanakimbia na kwenda Kipengere,Makete na halmashauri ya mji wa Njombe ambako tozo zake zipo chini,alisema Vasco Mgunda diwani kata ya Mfiriga"

Kufuatia mapendekezo hayo mwenyekiti wa halmashauri hiyo Valentino Hongoli akamtaka mkurugenzi wa halmashauri hiyo Sharifa Nabarang'anya kuja na mswada wa mabadiriko ya tozo na pia kubuni vyanzo vipya ili kutoa afuheni kwa wafanyabiashara na wakulima wa miti .

"Wakati naomba nafasi hii mwaka jana niliahidi kushghulikia kero hii ya tozo ya shilingi 200 kwa kila ubao kutokana na athari zake katika halmashauri hii ,hivyo namuagiza mkurugenzi katika robo ya pili ya mwaka aje na ripoti ya mapendekezo ya mabadiriko ya ushuru wa mbao.Alisema Valentino Hongoli diwani wa kata ya Ikunda na mwenyekiti wa halmashauri"

Katika hatua nyingine baraza hilo limeazimia mtendaji wa kata ya Ukarawa kuchukuliwa hatua kali ikiwemo kusimishwa kazi kabisa ili kuwa mfano kwa wengine kwakukiuka misingi na maadili ya utumishi wa umma na kushindwa kutekeleza majukumu yake kwasababu ya ulevi jambo ambalo linatolewa ufafanuzi na kaimu mkurugenzi.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post