Waandishi waaswa kujituma katika kazi, kuwa weledi

 Na Mapuli Misalaba, Shinyanga 


Waandishi wa habari wametakiwa kufanya kazi kwa bidii, kuwa wabunifu na kuzingatia weledi wa kazi ya uandishi ili kuleta mabadiliko chanya na kuepusha migogoro isiyo na tija katika jamii na Taifa kwa ujumla.


Wito huo umetolewa na Tatenda Nyayo, meneja wa kituo cha redio cha AFM kilichopo Dodoma,  katika mahafali ya nne (4) ya chuo cha uandishi wa habari na utangazaji cha Dodoma Media College.


Nyayo amewata wahitimu kutoridhika  na hatua hiyo ya kupokea vyeti na kuwasisitiza kuongeza maarifa huku akiwakumbusha kuwa wabunifu na kufanya kazi kwa bidii ili kuongeza thamani kwenye vyombo vya habari.


"Kila mtu anaweza akawa mwandishi wa habari kutokana na ukuaji wa Teknolojia lakini utofauti wenu utaonekana jinsi mtakavyozingatia weledi lakini yupo mtu akishapata cheti anafikiria ndo mwisho hapana mnatakiwa muendelee kuongeza maarifa muache tabia za kulizika kwenye media unapopata kazi unatakiwa uonyeshe uwezo wako ili kuwa mfanyakazi mzuri kwa kuongeza thamani kwenye vyombo vya habari kuwa waandishi wa mfano".


Akisoma historia fupi ya chuo hicho cha uandishi wa habari na utangazaji mkoani Dodoma, makamu mkuu wa chuo mipango, utawaka na fedha Vitus Lukebo amesema chuo hicho kilianzishwa rasmi Oktoba Mwaka 2017 kikiwa na wanafunzi 48 ambapo kufikia mwezi Oktoba Mwaka huu 2021 chuo kinajumla ya wanafunzi 695 katika fani ya uandishi wa habari na utangazaji.


Makamu mkuu wa chuo mipango, utawala na fedha Lukebo amesema jumla ya wahitimu wanaofanya maafali ya nne (4) Mwaka huu 2021 ni 113 kwa Astashahada (Certificate) na Stashahada (Diploma) huku akisema matarajio ya chuo katika ajira kwa wahitimu hao ni kuajiriwa na kujiajiri katika fani ya uandishi wa habari na utangazaji wa Runinga na Radio, kuwa maafisa habari, wapiga picha bora wa Magazeti na Runinga.


Lukebo amewaasa wahitimu kuzingatia Sheria na maadili ya taaluma kwa kuwaheshimu watu wote bila kujali vyeo, umri wala kipato hasa wazazi na walezi huku akisisitiza kwenda sambamba na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia.


"Zingatieni sheria na maadili ya taaluma hii pia muwaheshimu watu wote bila kujali cheo, umri wala kipato na hasa wazazi na walezi wenu ambao walijitolea sana kwa ajili ya elimu hii mliyoipata lakini pia mkumbuke kwenda sambamba na mabadiliko kasi ya Sayansi na Teknolojia".Maafali hayo ya nne (4) ya chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Dodoma yameambatana na zoezi la kutunuku vyeti maalum kwa wanafunzi wahitimu wa ngazi ya Astashahada (Certificate) na Stashahada (Diploma) waliofanya vizuri katika vipengele mbalimbali pamoja na utunukiaji wa uandishi wa habari na mawasiliano ya umma.Aidha Lukebo ameiomba serikali pamoja na taasisi zinazosimamia maendeleo ya elimu nchini kufanya kazi kwa ukaribu na vyuo vya kati ili kuvipa uwezo wa kufikia malengo kwa maslahi ya jamii na Taifa kwa ujumla.


Makamu mkuu huyo wa chuo mipango, utawala na fedha Lukebo ameongeza kuwa serikali iendelee kutilia mkazo suala la ajira kwa waandishi wa habari ikiwa ni sambamba na ofisi zote za serikali ikiwemo ofisi za mikoa, wilaya, kata, ofisi za mawaziri zihakikishe vinavitengo vya habari ili kuongeza wigo kwa waandishi wa habari.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post