UVCCM Dodoma waahidi kufuatilia kwa karibu miradi ya Serikali

 Na Rhoda Simba,Dodoma


KATIKA kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM, Umoja  wa Vijana wa Chama hicho (UVCCM) Wilaya ya Dodoma Mjini umesema utaendelea kufuatilia kwa karibu miradi ya Serikali huku wakitumia fursa hiyo kuwasaidia vijana kuweza kunufaika.


Aidha umoja huo umedhamiria kuhakikisha unawasaidia vijana kuwaunganisha na wadau mbalimbali ambao wanasimamia miradi ya Serikali kwa kuwapatia ajira zinazojitokeza kutokana na vigezo vyao jambo ambalo litasaidia kuwakwamua kiuchumi.


Hayo yamebainishwa jijini  hapa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi  (UVCCM )Wilaya ya Dodoma Mjini Said Kasote wakati wa ziara ya kukagua miradi mbalimbali ndani ya Wilaya ya Dodoma.


Katika ziara hiyo iliyowalenga Umoja wa Vijana UVCCM Mkoa wa Dodoma kutembelea Ofsi za umoja huo ngazi ya Wilaya kwa ajili ya kuwatembeza kwenye miradi ya Dodoma mjini kama inatekelezwa ipasavyo kupitia Ilani ya CCM ambayo inawataka viongozi wa chama kusimamia kwa ukaribu miradi ya Serikali na jinsi gani inawanufaisha wananchi.


Kasote akizungumza kwa nyakati tofauti amesema kuwa Uongozi na Timu waliyoambatana nayo wameridhishwa na hali inavyoendelea kwani wameona ni jinsi gani vijana wameshirikishwa kwenye miradi hiyo na mikopo ambayo inaenda kuwanufaisha wao na familia zao.


"Leo tumetembelea miradi ya Serikali tumeona vikundi vya vijana kata ya Nzuguni wakitengeneza majiko kupitia mikopo inayotolewa na halmashauri, Katika soko kuu la Job Ngugai wamepewa kipaumbele na wengine kuanzisha maduka ya simu,hotel ya nyota tano  jambo ambalo ndilo lengo la Serikali kupitia awamu ya sita sisi Umoja wetu kazi yetu ni kuhakikisha tunamuunga mkono Rais wetu Samia Suluhu Hassan kwa kusimamia miradi hiyo"  amesema Kasote.


Amesema kuwa vijana ambao wana changamoto ya ajira hasa wenye elimu na ambao hawana elimu ni wakati wao kuchangamkia fursa zinazotokana na miradi kwa kutoa ushirikiano,kudhubutu kazi wanazo ziweza bila kukataa tamaa jambo ambalo litasaidia kuinua uchumi wao .


Nae Katibu wa jumuiya hiyo Ahmed Kibamba amesema miradi hiyo yenye thamani kubwa ametumia fursa hiyo kuwasihi Vijana kuacha dhana potofu kwamba wenye elimu ndiyo wanapewa kipaumbele kitendo ambacho kinaweza kuwasababishia kukosa fursa kutokana na mawazo yao potofu.


Prisca  ni kijana wa umoja huo akiwa kwenye ziara hiyo amesema Chama Cha Mapinduzi kiendelee kuwashika mkono Vijana walioko pembezoni ambao wengi hawaelewi wapi pa kuanzia kupata ajira .


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post