Wataalam Ujenzi na TANROADS yawataka wananchi kujenga mbali na barabara kuepuka ajali

Zafarani Madayi, Meneja mazingira Wakala wa barabara nchini TANRODS, akijibu maswali ya Mabalozi wa usalama barabarani(RSA) kutoka mikoa mbalimbali nchini walipotembelea banda la wizara ya ujenzi

 

Na Seif Mangwangi, Arusha

WAKAZI wanaoishi pembezoni mwa barabara wametakiwa kufuata sheria za usalama barabarani kwa kutojenga nyumba karibu na barabara ili kuepuka ajali za mara kwa mara ambazo zimekuwa zikitokea katika maeneo yao.


Wito huo umetolewa jana na Zafarani  Madayi Meneja kitengo cha mazingira usalama barabarani wa wakala wa barabara nchini (TANROADS), ambae amesema wamekuwa wakilazimika kujenga matuta barabarani ili kupunguza ajali za mara kwa mara.


Amesema kiuhalisia, barabara kuu (high way), kwa kawaida hazipaswi kujengwa matuta barabarani lakini kutokana na uelewa mdogo wa matumizi ya barabara TANROADS wamekuwa wakilazimika kujenga matuta ili kupunguza ajali.


Akijibu maswali mbalimbali ya mabalozi wa usalama barabarani waliotembelea banda la wizara ya ujenzi katika maonyesha ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani katika viwanja vya shekh Amri Abeid Arusha, Zafarani Madayi amesema TANROADS imekuwa ikihakikisha mazingira ya barabara yanakuwa salama wakati wote.


Amesema katika maonyesho hayo wamekuja kuonyesha kazi mbalimbali zinazofanywa na TANROADS ikiwemo ujenzi wa barabara unaoendelea ikiwemo barabara ya mzunguko wa Dodoma, Rusaunga Dodoma, Daraja la Tanzanite(Salander Bridge), daraja la Kigogo-busisi pamoja na ujenzi wa viwanja vya ndege.


“ Tumeweza kuandaa kazi mbalimbali ambazo TANROADS inazifanya, wananchi wakija hapa wataelewa kazi zetu na kujifunza umuhimu wa kutunza barabara,”amesema.


Akijibu swali kutoka kwa mabalozi wa usalama barabarani, kuhusu madai ya kwanini madereva wasiruhusiwe kupima mizani moja pekee badala ya kupima kila kituo, mtaalam wa mizani kutoka wizara ya ujenzi na uchukuzi, Mhandisi Leonard Saukwa amesema kumekuwa na sababu mbalimbali za kupima uzito wa magari ikiwemo kupata takwimu za wingi wa magari ili kuboresha huduma za barabara.


Mhandisi Leonard Sauko akijibu maswali ya Mabalozi ya usalama barabarani kuhusu matumizi ya mizani za kupimia magari ya mizigo na abiria barabarani

Pia amesema madereva wengine wamekuwa sio waaminifu ambapo baada ya kupima mizani moja huongeza mzigo lakini pia wakati mwingine mzigo hucheza na hivyo uzito kuongezeka tofauti na vipimo vya awali.


“Katika vipimo vya mizani, tumeweka asilimia 5 ya ziada ili kusaidia kama mzigo utacheza basi itafidia kwenye hiyo asilimia5, lakini utakuta mfanyabiashara yeye anajaza hadi zile asilimia5 za ziada ambazo sisi tumemuwekea, akija akikutwa mzigo umezidi anapigwa faini anaanza kulalamika, niwaambie tu kwamba sisi sio wakorofi wafuate sheria tu,”anasema.


Anasema faini ambayo imekuwa ikitozwa kwa magari yanayoongeza uzito ni kwaajili ya kusaidia kurudisha eneo ambalo limeathirika na sio mapato ambayo Serikali imekuwa ikiyapata hivyo watu wanatakiwa kufanya matumizi sahihi ya barabara ili kuepuka faini hizo.

 

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post