PUMA yadhamini mashindano ya kuchora picha za usalama barabarani, yatoa zawadi kwa washindi

Mkuu wa Wilaya Dodoma Mjini, Jabir Shekimweri (kulia) akikabidhi kikombe cha ushindi wa kwanza kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Chidachi, Veronica Suya na Diwani wa Kata ya Dodoma Makulu, baada ya mwanafunzi wa shule hiyo Joseph Thadei kuibuka  mshindi wa mashindano ya kuchora picha zinazoonesha mambo ya usalama barabarani. Mashindano hayo yaliyoshirikisha wanafunzi wa shule mbalimbali za jiji hilo yaliendeshwa na Taasisi ya Amend kwa udhamini wa Kampuni ya Mafuta ya Puma. Mwanafunzi huyo amezawadiwa sh 500,000 na shule sh. mil. 4. Hafla hiyo imefanyika katika shule ya Msingi Kisasa jijini Dodoma Novemba 2,2021. 
Mshindi wa pili wa mashindano hayo Emmz Martine kutoka Shule ya Msingi Kisasa, akipokea cheti  kutoka kwa Mkuu wa Wilya, Shekimweri.
Mwanafunzi Joseph Thadei wa Shule ya  Msingi Chidachi akipokea cheti kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Jabiri Shekimweri baada ya kuwa mshindi wa kwanza katika mashindano hayo. Mwanafunzi huyo amezawadiwa sh. 500,000.
Mkuu wa Wilaya, Jabiri Shekimweri  akiwa na viongozi wengine meza kuu wakikagua picha zilizopata ushindi wa kwanza hadi wa kumi.Kutoka kushoto ni  Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Leonce Kaimukirwa Mwakilishi wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Diwani wa Kata ya Dodoma Makulu na Meneja wa masuala ya sheria wa Kampuni ya Puma, Godluck Shirima.
Baadhi ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali zilizoshiriki mashindano hayo.
Walimu wakicheza kwa furaha baada ya wanafunzi wao kutangazwa washindi.
Mkuu wa Wilaya, Shekimweri na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na  washindi mara baada hafla ya kuwakabidhi tuzo kumalizik

 Na Mwandishi Wetu, Dodoma


MKUU wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri ameipongeza Kampuni ya Puma na AMEND kwa kuendesha mafunzo ya usalama barabarani kwa zaidi nya wanafunzi 120 katika mikoa mitano nchini ambayo anaamini yatachangia kupunguza ajali za barabarani ambazo wahanga wakubwa ni Wanafunzi.

KATIKA kuhakikisha ajali za barabarani zinapungua, zaidi ya Wanafunzi 120,000 Nchi nzima wamepatiwa mafunzo ya usalama barabarani Ili kuweza kutokomeza ajali hizo.

Pongezi hizo amezitoa wakati wa hafla ya kufunga Mafunzo hayo jijini Dodoma leo ambayo yameendeshwa na Kampuni ya Mafuta ya Puma kwa kushirikiana na Shirika lisilo la Kiserikali la AMEND.

Mikoa iliyoshirikishwa kwenye mafunzo hayo ni Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, Geita, Ruvuma na Kilimanjaro pamoja na visiwani Zanzibar.

DC Shekimweri amesema kuwa anatambua mbali ya kutolewa elimu ya barabarani, wameendesha shindano la mchoro wa usalama barabarani, na hivyo ameamua kuongeza zawadi kwa mshindi wa shindano hilo."Nitatoa Sh.100,000 na wengine naomba mchangie,walimu hawa ambao wanafundisha elimu ya usalama barabarani na kuwafundisha kuchora nao wapate motosha.

Katika mashindano hayo ya michoro, Mwanafunzi kutoka Shule ya Msingi Chidachi, Joseph Chidachi amejinyakulia kiasi cha Sh Laki Tano huku Shule yake ikipata Sh Milioni Nne huku Shule ya Kisasa ikishika nafasi ya pili na ya tatu.

" Niwapongeze sana Puma na AMEND jambo hili mlilolifanya ni kubwa na lenye manufaa makubwa kwa Taifa letu, elimu hii itawajengea uelewa vijana wetu juu ya usalama barabarani na hivyo kupunguza ajali nyingi ambazo zimekua zikileta vifo kwa wanafunzi wetu, walemavu na hata watembea kwa miguu wengine.

Nitumie fursa hii kuliagiza Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani jijini Dodoma kushirikiana na Shule zetu kuendesha mafunzo kwa wanafunzi wetu na kuwapatia vifaa kwa ajili ya wanafunzi wanaosimama barabarani kuzuia magari wenzao wapite," Amesema DC Shekimweri.

Ametumia fursa hiyo kumshukuru Rais Samia kwa miundombinu ya barabara katika Jiji la Dodoma na hivi karibuni Sh.bilioni 300 zimetengwa kwa ajili ya miundombinu na wamepanga  kujenga pia barabara za pande mbili ambazo zote zitazingatia watembea kwa miguu pamoja na alama za barabarani.

"Takwimu za watu wanaopata ajali za barabarani bado ni kubwa, nafikiri kuna haja ya kuongeza elimu ili kupunguza au kuondoa kabisa vifo vya watoto, wazee na wenye ulemavu.Nawaagiza Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani jijini Dodoma kuongeza mafunzo kwa wanafunzi ambao wamekua wakisimama barabarani kuzuia magari ili wanafunzi kuvuka sambamba na kuwapatia vifaa.

" Tutaendelea kusimamia sheria ya usalama barabarani, nitoe rai kwa Jeshi la Polisi kuwa wakali kwa wanaovunja sheria za barabarani, haiwezekani mtu anatembea mwendo kasi sehemu ambayo kibao kinamuonesha kutembea mwendo mdogo,  na Polisi mkimkamata mtu mara nyingi zaidi basi ikiwezwkana anyang'anywe leseni yake," amesema Shekimweri.

 
Ofisa Uhusiano wa Puma, Godluck Shirima akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Puma, Dominic Dhanah ameishukuru Serikali kwa namna ambavyo wametoa ushirikiano kwao wakati wa utekelezaji wa mafunzo hayo huku akiahidi kuwa wataendelea kutoa mafunzo hayo kwa wanafunzi lengo likiwa ni kutokomeza kabisa ajali za barabarani.

Amesema utoaji wa zawadi hizo unahitimisha mradi uliotekelezwa na Puma na Amend ambao ulihusisha mafunzo kuhusu usalama barabarani na uchoraji wa picha kwa shule za Kisasa, Ipagala B, Chidachi, Makole na Dodoma Mlimani ambapo wanafunzi wasiopungua 20,000 walipata mafunzo hayo.

“Huu mpango huu wa usalama barabarani ni mwendelezo wa kampeni ambayo ilizinduliwa rasmi miaka tisa iliyopita ambapo zaidi ya shule 100 zimefikiwana na wanafunzi zaidi ya 120,000 mikoa mbalimbali wamepata mafunzo hayo,”alisema.

Amesema kwa njia hiyo Puma Energy inaamini kuwa watoto watakuwa salama na kutakuwa na taifa lenye watu imara na wenye nguvu za kulitumikia taifa lao.

" Lengo letu kama kampuni ni kuongeza wigo ili kufikia shule nyingi zaidi nchi nzima kwa mwaka 2022, sisi kampuni ya Puma Energy tunaahidi kuendelea kuwekeza katika kampeni ya usalama barabarani kwa kushirikiana na serikali kupitia jeshi la Polisi ili kuokoa maisha ya watanzania,” Amesema Shirima.

Nae Mkaguzi  Msaidizi wa Polisi ambaye amemwakilisha Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Leonce Kaimukirwa amesema wamefurahishwa na mafunzo ambayo yamekuwa yakitolewa na Amend kwa kushirikina na Kampuni ya Puma Energy Tanzania na kwamba Jeshi la Polisi limekuwa likitoa mafunzo ya usalama barabarani.

"Tumekuwa tukitoa elimu katika shule za msingi,shule za sekondari ,vyuoni pamoja na watumiaji vyombo vya moto wakiwemo waendesha bodaboda,  tumekuwa tukielimisha wazazi kutopakia watoto wao kwenye bodaboda,tunawashauri wazazi wasikubali watoto kubebeshwa zaidi katika bodaboda,"amesema.

Amefafanua mafunzo hayo yamekuja wakati muafaka na kuongeza kauli ya Jeshi la Polisi katika kuelekea Wiki ya Usalama Barabarani inasema Jali maisha yako,jali maisha ya wengine."Hivyo kwetu mafunzo haya ni muhimu sana , ni muhimu tukashirikiana kwa ajili kupunguza ajali."

Simon Kalolo ambaye ni Meneja Mkuu wa Shirika lisilo la kiserikali la  Amend Tanzania, amesema wamekuwa wakitekeleza miradi mingi katika nchi zaidi ya 10 barani Afrika ikiwemo Tanzania.

"Moja ya mradi ambao tunautekeleza ni mradi wa elimu ya usalama barabarani, ajal bado ni changamoto, duniani watu zaidi ya 350,000 wanapoteza maisha na wengine zaidi ya milioni  tatu wanabakiwa na ulemavu wa  hivyo jitihada zinahitajika, mbali ya elimu pia kumefanyika mashindano ya michoroya usalama barabarani.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post