Mkurugenzi Kibaha aingilia kati mgogoro wa makazi Mitamba

Mkurugenzi wa Mji mdogo Halmashauri ya Kibaha Mshamu Alli Munde


Na Mwandishi Wetu,Pwani

MKURUGENZI wa Mji mdogo Halmashauri ya Kibaha mkoani Pwani Mhandisi Mshamu Alli Munde  amewataka wakazi wa Mitamba kuwa na subira katika utatuzi wa suala lao la makazi.


Mkurugenzi huyo amezungumzia sakata hilo ofisini kwake alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kufuatia malalamiko ya wakazi wa Mitamba kulalamikia alama za kubomoa makazi yao ili hali serikali ilielekeza kutuma timu maalumu kuchunguza mgogoro huo wa muda mrefu


Mshamu amesema kila mmoja anafahamu alama hizo lazima ziwekwe kwa kuwa baadhi ya wakazi hao wameanza kuyauza maeneo hayo kwa watu mbalimbali kinyume na utaratibu waliopewa na serikali, amesema katika kikao cha mwisho wakichofanya katika eneo hilo wakazi hao walikiri kuwa walivamia eneo hilo na kujenga makazi yao ya kudumu bila kuuliza kwa mamlaka husika


"Kwa kuwa wananchi walivamia na kuishi kwenye eneo hilo, lakini waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi William Lukuvi alishaunda tume kuchunguza na kubaini jambo hilo, hivyo hakupaswi mtu yeyote kuendeleza ujenzi au kumuuzia mtu mwingine eneo, na kwa kufanya hivyo huo ni wizi wa mchana" alisema


Aidha mkurugenzi huyo ametoa rai kwa wakazi wa Halmashauri ya kibaha kuhakikisha wanafika katika ofisi za mkurugenzi kuhakiki maeneo yao kabla hawajawapa ela matapeli wanauza ardhi s eneo ambalo linamilikiwa na serikali 


Baadhi ya wananchi wameelekeza malalamiko yao kwa serikali kwa kushindwa kuliendeleza eneo hilo ambako kulisababisha wananchi wengi kuvamia eneo la Mitamba


Alhaji Khamisi mkazi wa eneo la Mitamba amesema mkuu wa Wilaya aliahidi kuja kuleta majibu kama alivyoelekezwa na Waziri wa Ardhi lakini yeye akaja kuweka alama za bomoa, mkazi huyo ameomba Waziri kufika kutatua mgogoro huo mapema badala ya kuongeza misuguano baina ya Serikali na wananchi


Naye Halima Hamid amesema serikali ilifika katika eneo lao na kuwapatia namba pamoja na kuwapiga picha, wakasema kila mwananchi ajenge kwa tofari za block, lakini Leo wanageuka kutufukuza bila kurudi kwenye makubaliano ya awali, swali hapa tunauliza, Je ni kwanini serikali ilitupatia namba pamoja na kutupiga picha kwa nia ya kutathmini makazi yetu? Alama za kubomoa kwanini zije wakati huu ambao tume inachunguza jambo letu?

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post