Kampuni ya Bima Britam mahakamani kushindwa kumlipa mteja Mil100

 Kampuni ya bima ya Britam Tanzania Limited,imefikishwa mahakamani kwa kushindwa kumlipa fidia.

 mfanyabiashara,James Rugangira(43), mkazi wa Moshono jijini Arusha baada ya kupata ajali mbaya iliyosababisha kufanyiwa upasuaji mkubwa wa kichwa akiidai imlipe kiasi cha sh, milioni 100.


Mfanyabiashara huyo, alifungua kesi ya madai namba 07/2021, Februari 02 mwaka huu, katika mahakama ya
Wilaya ya Arumeru, na imepangwa kuanza kusikilizwa desemba mosi mwaka huu, mbele ya Hakimu wa mahakama hiyo,Amalia Mushi.


Awali kesi hiyo, ilipangwa kusikilizwa leo katika mahakamani hiyo, lakini iliahirishwa kwa kuwa hakimu huyo alipata udhuru.

Rugangira ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya ulinzi ya Geo Limited,katika shauri hilo,alidai kwamba amefungua kesi hiyo, kwa kuwa kampuni hiyo ya bima ilishindwa kumlipa fidia baada ya kupata ajali akiwakwenye gari aina ya Rav 4 lenye usajili wa namba T828 DGN Mali ya Eunice Mrema lililokuwa likiendeshwa na Ally Msungi.

Alidai kwamba baada kutokea kwa ajali hiyo Julai 1 2019, kampuni ya bima ilitakiwa kumlipa fidia ya Sh.milioni 20 kwa ajili ya matibabu aliyopatiwa katika Hospitali ya Aga Khan,Nairobi nchini Kenya.

"Baada ya kukaa muda mrefu ya bila kufanya kazi kutokana na ajali gharama alitakiwa kulipwa Sh.milioni 20, lakini kwa kuwa walishindwa kumlipa awali gharama zimeongezeka Sh.milioni 20 nyingine kutokana na kesikufika mahakamani.

Vile vile mlalamikaji huyo, alidai kwamba kampuni hiyo inapaswa kumlipa gharama za uathirika alioupata kwa kipindi chote kiasi cha Sh.milioni 100.

"Washtakiwa katika kesi hii, wameshindwa kunifidia gharama zangu baada ya kupata ajali ambayo ilisababisha mimi kutumia fedha nyingi kufanyiwa upasuajia wa kichwa Nairobi katika Hosiptali ya Aga Khan,”alidai.

Alidai kutoka na ukubwa wa bima iliyokatiwa gari hilo lililopata ajali inaruhusu kulipwa hadi Sh.milioni 60, lakini kampuni hiyo ilikuwa tayari kumlipa Sh.500,000 hivyo alikataa fedha hizo na kuamua kufungua kesi hiyo katika mahakama hiyo.

Katika shauri hilo la madai mfanyabiashara huyo, amemshitaki Eunice Mrema ambaye ni Mmiliki wa gari lililopata Ajali kama mshtakiwa namba moja na anawakilishwa na Wakili Mosses Mahuna.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi desemba mosi mwaka huu itakapokuja Kwa ajili ya usikilizwaji.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post