Kampuni mpya ya bima yaingia nchini, yajivunia historia nzuri ya utendaji

 


Mwenyekiti wa kampuni ya bima ya Grand Re Tanzania,Shinganyi Mutasa (kushoto) akimkabidhi zawadi ya kumbukumbu Kamishna wa Bima nchini , Dk. Mussa Juma, ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampuni hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Kamishna wa Bima nchini , Dk. Mussa Juma, akibadilishana mawazo na mwenyekiti wa kampuni ya Mac Group, Yogesh Manek (katikati) , kulia ni mmoja wa wakurugenzi wa Masawara Financial Services.
Mwenyekiti wa kampuni mpya ya bima ya Grand Re Tanzania, Shinganyi Mutasa, akielezea huduma za kampuni hiyo kwa wageni waalikwa wakati wa hafla ya uzinduzi wake iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wageni waalikwa waliofika kwenye hafla ya uzinduzi wa kampuni mpya ya bima ya Grand Re wakifuatilia hotuba.
Baadhi ya wageni waalikwa waliofika kwenye hafla ya uzinduzi wa kampuni mpya ya bima ya Grand Re wakifuatilia hotuba.

***

Kampuni ya Grand Re inayoongoza kutoa huduma za Bima barani Afrika ikiwa na mtandao wa matawi yake katika nchi mbalimbali ya Afrika nzima, imezindua huduma zake nchini Tanzania.

Grand Re, ilianzishwa rasmi mnamo mwaka wa 2005, ikiwa na lengo ya kutoa huduma bora za bima za aina mbalimbali katika soko la Afrika hususani katika nchi zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Kampuni hiyo imekua kwa kiasi kikubwa, na kuwa chaguo la wateja wengi katika nchi mbalimbali barani Afrika, ikiwa na matawi mengi yanayotoa huduma katika nchi za Zimbabwe na Botswana, na sasa imeingia Tanzania kwa ajili ya kutoa huduma bora za bima.

Kampuni ya Grand Re ni kampuni tanzu inayomilikiwa na kampuni ya Masawara Investments Mauritius Limited, inayotoa huduma mbalimbali zaidi ikiwa imejikita katika sekta za kifedha, uwekezaji, TEHAMA, na hoteli.

Mwenyekiti wa kampuni hiyo Shinganyi Mutasa, alisema wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika jijini Dar es Salaam, kwamba kampuni hiyo inatoa huduma za bima ya uhakika na za kifedha hususani katika nchi zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara kupitia kufanya kazi pamoja kwa ubunifu, uadilifu, kuaminika na shauku ya kutoa huduma bora kwa wateja.

Grand Re Tanzania, iliyoaza kutoa huduma chini katika siku za karibuni ikilega soko la nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, itatoa huduma mbalimbali za bima zikiwemo bima za muda mfupi za kukabiliana na majanga ya usafiri wa anga, moto, magari na nyinginezo.

Kampuni pia inajihusisha na ushauri wa kitaalamu wa kukabiliana na majanga mbalimbali,usalama wa kifedha lengo likiwa ni kuwawezesha wateja wake kufanya biashara zao kwa kujiamini zaidi na kupata mafanikoa katika biashara zao.

Akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi, Kamishna wa Bima nchini, Dk. Musa Juma, ambaye alikuwa mgei rasmi, aliipongeza kampuni ya Grand Re, kwa kufungua tawi nchini Tanzania a kuongeza kuwa anaamini kuwa itatumia uzoefu wake mkubwa na utaalamu kuzidi kuboresha huduma katika sekta ya bima nchini. 

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post