Akutwa amekufa chini ya daraja

 Na Mapuli Misalaba, Shinyanga


Mtu mmoja mwanaume anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 35 na 40 asiyefahamika jina wala makazi yake, amekutwa amefariki Dunia chini ya daraja la Ndala katika Manispaa ya Shinyanga 


Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi wa Polisi George Kyando amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kubainisha kuwa, baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema alituma askari kwenda kwenye eneo la tukio ambao walikuta mwili wa marehemu ukiwa chini ya daraja lakini haukuwa na jeraha lolote.Amesema kwa sasa mwili wa marehemu uko katika Hosptali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kitabibu  ili kubaini chanzo cha mtu huyo.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post