Wazazi watakiwa kuwekeza kwenye elimu za watoto wao ili waweze kutimiza ndoto za kufanya vizuri katika mitihani yao

 Na  Mapuli  Misalaba,  Shinyanga

Mkuu  wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amewaomba wazazi na walezi kuwasimamia watoto wafikishe ndoto zao kwa kuwekeza kwenye elimu ikiwa ni pamoja na kushirikiana na walimu na kufuatilia maendeleo  yao ili wakawe na vipato vyao kuliko kuwa tegemezi

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko


Ameyasema hayo leo kwenye mahafali ya tano ya ya darasa la saba ambapo pia ni maafali ya 10 kwa darasa la awali katika shule ya msingi Little treasures ambapo amesema wazazi wana wajibu mkubwa  wa kushirikiana na walimu ili kutimiza ndoto za watoto


Mboneko ambaye pia alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali hayo amewaomba wazazi kutowazuia watoto vipaji vyao na kulitilia manani suala la elimu ikiwa ni pamoja na kuhudhuria vikao vya wazazi shuleni ili kusikiliza na kufahamu maendeleo ya watoto

  

 “Niwaombe sana wazazi tusiwazuie watoto kwenye vipaji vyao watoto hawa mmewaona wanavipaji lakini darasani wanafanya vizuri tuendelee kutia manani suala la elimu watoto wamesema umuhimu wa elimu inatengeneza watoto inatoa wataalam mbalimbali na wao wanataka kufikia ndoto zao wazazi tutoe ushirikiano kwenye shule zetu na tuwe na muamko wa kuja kwenye vikao vya wazazi kusikiliza maendeleo lakini pia kufuatilia maendeleo ya watoto shuleni”


Amewaomba wazazi kutia msukumo mkubwa kwa watoto katika elimu kwa kuwasimamia na kuwaombea pamoja na kuwafundisha uzalendo na utamaduni kwa kuendelea kujenga Taifa la Tanzania 


“Wazazi tuwasimamie watoto wafikishe ndoto zao na hakuna urithi mzuri kwa mtoto kama elimu tukiwapeleka shule watakwenda kufanya kwa bidii, kusoma kwa bidii ili wawe na vipato vyao kuliko kuwa tegemezi tupeleke watoto shule na wao wakawe watu wazuri kulijenga Taifa lakini tuwafundishe uzalendo na utamaduni tutie msukumo mkubwa kwenye elimu tuwasimamie na kuwaombea maana bila mwenyezi Mungu hakuja jambo litakalo kwenda vizuri lakini kwa darasa la saba waliomaliza wazurulaji kwenye mitaaa yetu watulie nyumbani na wazazi tuwalee vizuri”


Kwa upande wake mkurugenzi wa shule ya msingi na Sekondari Little treasures Lucy Msele amewaomba wazazi kuendelea kushirikiana na walimu katika suala la makuzi na malezi ya watoto 


“Tuendelee kuombeana na kulea watoto wetu vizuri tukisirikana na walimu pamoja na wazazi lengo ni kutoa watoto ambao watakuwa wazuri kwa upande wa wanafunzi wetu wa darasa la saba tumeishi taku wazazi walipowaleta na kutukabidhi leo mmemaliza mkawe watoto watiifu kwenye familia, jamii na sehemu yeyote ile”


Naye meneja wa shule ya msingi na Sekondari Little treasures iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga Willykled Mwita amesema wamefanya ditihada mbalimbali kuhakikisha wanafunzi wote wanakuwa wanafunzi bora hasa kwenye taaluma ya elimu 


Mwalimu mkuu wa shule ya msingi  Little treasures Paul Kiyondo akisoma lisala ameeleza historia fupi ya shule hiyo 

“Leo ni  maafali ya tano kwa wanafunzi 98 wavulana 54, wasichana 44 wa darasa la saba pia ni maafali ya kumi kwa wanafunzi 87 wavulana 48, wasichana 39 wa darasa la awali wahitimu wote hawa wameandaliwa vizuri kujiunga na kidato cha kwanza na darasa la kwanza mwaka ujao 2022”

“Sambaba na maafali shule yetu imetimiza miaka kumi tangu kuanzishwa kwake na hivyo tumeanza kuadhimisha kwa kufanya shughuli mbalimbali za kiutu kwa kutembelea vituo mbalimbali vinavyolea watu wenye uhitaji maalum baadhi ya vituo hivyo ni Chibe, Buhangija, Busanda na Kolandoto pia tulifanya shughuli za usafi wa mazingira nje  na ndani ya shule. Katika kipindi kikubwa tangu kuanzishwa kwa shule yetu tumekuwa na mafanikio makubwa sana katika nyanja mbalimbali kama vile taaluma, malezi, miundombinu, mazingira, afya, usalama wawanafunzi na walimu kitaaluma shule yetu ipo katika kiwango cha juu sana kwa ufaulu wawanafunzi katika mitihani ya Taifa kwa darasa la nne na darasa la saba”

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post