Watakiwa kuzingatia sheria, kuepuka migogoro ya ardhi

 Na  Mapuli  Misalaba,  Shinyanga

Wakazi wa Manispaa ya Shinyanga wametakiwa kuzingatia Sheria,kanuni na taratibu zinazotolewa na idara ya ardhi, katika  umiliki wa ardhi ili kuepusha migogoro inayoweza kuzuilika

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Idara ya ardhi Manispaa ya Shinyanga, Salu Ndongo ambapo amesema migogoro inayojitokeza mara kwa mara imekuwa ikisababishwa na Wananchi kutozingatia sharia na kanuni za umiliki wa ardhi

Ndongo amewaomba wananchi kuendelea kuishi vizuri na majirani, kuishirikisha serikali ya mtaa katika hatua ya kuuza au kununua ardhi na kuacha tabia ya kuuza  ardhi kienyeji 

“Ishi vizuri na majirani kwa sababu ndiyo wanaoweza kukusaidia kutatua migogoro na majirani wa kwanza ni serikali ya mtaa ukitaka kununua eneo serikali ya mtaa inakuwepo kwa sababu ukipatwa na tatizo umevamiwa au kunalolote limetokea wakwanza  kukusaidia ni jirani yako wito wangu watu wafuate sheria wasiuziane ardhi kienyeji na wawe watiifu kwenye sheria  kimsingi sisi tukotayari kutoa huduma kwa wananchi bila upendeleo hatujari rangi ya mtu, uwezo wa kifedha kwa sababu tunalipwa mshahara kwa kuwahudumia watu wa aina zote”


Afisa huyo amesisitiza umuhimu wa kuishirikisha idara ya ardhi katika suala zima la umilikiwa ardhi hasa pale Watu wanapouziana kiwanja,shamba au nyumba.

“Ili kuepusha migogoro ya ardhi watu waje kufuatilia kabla hawajanunua maeneo waje ofisini kwanza ili wajilidhishe kwamba hakuna mgogoro kitu kingine ni vizuri wananchi wakaheshimu ramani kwa sababu zimezingatia sheria kama mwananchi hatoridhika kwa mujibu wa sheria za ardhi serikali inautaratibu na namna ya kutafuta haki ataenda kwenye baraza la ardhi la kata kwa mali ambazo zinathamini kuanzia  Milioni tatu kushuka chini, baraza la ardhi na nyumba la wilaya kwa mali ya ardhi yenye thamani zaidi ya Milioni tatu kwenda juu”

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post