Walengwa Tasaf walia na mfumo mpya wa kielektroniki

 Na Mapuli Misalaba, Shinyanga


Baadhi ya walengwa wa mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF katika Manispaa ya Shinyanga wameiomba serikali kuangalia namna bora ya kuwapatia ruzuku yao ambayo wanakwama kuipata kutokana na mfumo wa kielekitroniki unaotumika hivi sasa kuwa na changamoto.


Wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauti  wazee wa vitongoji vya Mwasele B na Mwasele Mihogoni Kata ya Kambarage wamesema kuwa mfumo huo wa kutumia alama za vidole umekuwa ukiwakwamisha baadhi ya wazee ambao alama hizo hazisomi kwenye mfumo huo.


Wamesema mpaka sasa wameendelea kuishi maisha ya tabu ikiwa ni pamoja na kukosa chakula hivyo wameiomba serikali kuchukua hatua za haraka kutatua changamoto hiyo ili kuwawezesha kupata ruzuku hiyo.


Kwa upande wake mwenyekiti wa Kitongoji cha Mwasele Mihogoni Bwana Richard Baluhi amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo ambapo ameshauri kuendelea kutumika kwa mfumo wa zamani kwa kuwa utaratibu unaotumia hivi sasa wa kwenda benk haujazoeleka kwa wengi wao.

Baluhi amesema changamoto hiyo inawakabili zaidi ya walengwa 15 wa mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF katika kitongoji chake cha Mwasele Mihogoni ambapo amesema ni awamu nne zimepita zote hawajapatiwa ruzuku hiyo.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post