Ujenzi vyumba vya madarasa kuchochea ufaulu wanafunzi shinyanga

 Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Wanafunzi wa shule ya Sekondari Mazinge iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga wameishukuru serikali, kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ambapo kukamilika kwake itasaidili kuweka mazingira bora na salama kwa Wanafunzi kujifunzia lakini pia walimu kufundishia

Wamesema  kuwa  ujenzi wa vyumba vya madarasa ni hatua itakayochochea ufaulu kwa wanafunzi ambapo watajisomea kwa bidii na kuhudhuria  ratiba za masomo

Wanafunzi hao wamewashukuru Wazazi,walezi na jamii iliyofika shuleni hapo leo kwa ajili ya kushiriki shughuli ya kuchimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili  vya madarasa,ikiwa ni jitihada za kuunga mkono juhudi za serikali

Wakizungumza wakati zoezi la kuchimba msingi likiendelea baadhi ya Wazazi wameipongeza serikali kwa jitihada zake mbalimbali zilizolenga kuboresha miundombinu katika sekta ya elimu, ambapo wamewataka Wanafunzi kuongeza jitihada katika masomo ili waweze kufikia malengo waliyokusudia

Kwa upande wake diwani wa kata hiyo ya Ndembezi Victor Tobias Mmanywa ametoa wito kwa wazazi na walezi kusimamia na kuhakikisha wanafunzi wanahudhuria shuleni ili waweze kufaulu mitihani hayo na kufikia malengo yao

“Wazazi tuhakikishe watoto wetu wanaenda shule ili waweze kufaulu mitihani kwa ajili ya kesho yao kwa sababu utoro unachangia kushuka kwa kiwango ifike sehemu mwanafunzi lazima wakasilikiwe ili waweze kusonga mbele lengo ni kufanikisha Taifa liwe na watu wanao jitambua pia walimu nao wanatakiwa kuwasimamia kweli kweli wanafunzi ili wafaulu”

Diwani huyo ambaye ni siku yake ya kwanza kuwajibika kwa kukutana na wananchi wa kata yake na kushiriki shughuli kwa pamoja 

Naye  mkuu wa shule hiyo James Msimba amesema fedha za ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa itasaidia kupunguza changamoto ya upungufu wa madarasa,na kuongeza ari ya wanafunzi kujisomea na kuhudhuria masomo,lakini pia Walimu kufundisha katika mazingira bora

“Shule yetu imapatiwa fedha shilingi Milioni 40 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa viwili, shule inajumla ya wanafunzi 778 na tunauhitaji wa vyumba vya madarasa 20 ongezeko la vyumba viwili ambavyo tumepatiwa itatusaidia kwa sehemu kubwa sana kupunguza changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa”

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post