St.Anne Marie Academy yatoa mwanafunzi bora kitaifa

Mwanafunzi bora wa kitaifa kwenye matokeo ya darasa la saba kutoka St Anne Marie Academy ya Mbezi Kimara kwa Msuguri Eluleki Haule akiwa na mama yake kwenye mahafali ya darasa la saba ya shule yaliyofanyika hivi karibuni shuleni hapo.


Mwanafunzi bora wa kitaifa kwenye matokeo ya darasa la saba kutoka St Anne Marie Academy ya Mbezi Kimara kwa Msuguri Elulek  Haule akiwa na keki yake alipkuwa kwenye mahafali ya kumaliza darasa la saba yaliyofanyika mwezi wa kumi mwaka huu.
Mwanafunzi bora wa kitaifa kwenye matokeo ya darasa la saba kutoka St Anne Marie Academy ya Mbezi Kimara kwa Msuguri Elulek  Haule akiwa amebebwa na wenzake mara baada ya kutangazwa mshindi kitaifa kwenye matokeo ya darasa la saba mwaka huu
Mwanafunzi bora wa kitaifa kwenye matokeo ya darasa la saba kutoka St Anne Marie Academy, ya Mbezi Kimara kwa Msuguri Eluleki Haule akiwa amebebwa na wenzake kwa furaha mara baada ya Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), kumtangaza kuwa mwanafunzi bora kitaifa.

       

Na Mwandishi Wetu


SHULE ya St. Anne Marie Academy ya Mbezi Kimara kwa Msuguri jijini Dar es Salaam, imefanikiwa kutoa mwanafunzi bora kitaifa kwenye matokeo ya darasa la saba yaliyotangazwa mwishoni mwa wiki.

Mwanafunzi huyo aliyeibuka kidedea kitaifa kutoka shule hiyo ni Eluleki Haule kutoka shule ya St Anne Marie Academy, ambaye amesema ndoto yake ni kuwa mpelelezi na kufanyakazi kwenye Idara ya Usalama wa Taifa (TISS).


Akizungumza na gazeti hili mjini Bagamoyo anakosoma masomo ya kujiunga na kidato cha kwanza kwenye shule ya Mariab Boys, Eluleki alisema amekuwa na ndoto hiyo ya kuwa mpelelezi kwa muda mrefu.


Alisema awali ndoto yake ilikuwa kuja kuwa rubani wa ndege kubwa kubwa lakini alibadili ndoto hiyo na kwa sasa hamu yake kubwa ni kufanya kazi ya upelelezi.


“Awali nilikuwa natamani sana kufanyakazi ya urubani na kwa kweli ilikuwa shauku yangu ya muda mrefu lakini hivi karibuni nimeona nibadili sasa natamani kuwa mpelelezi tu,” alisema Eluleki ambaye alisema atasomea masomo ya Fizikia, Kemia na Hisabati.


Alisema siri ya ufaulu wake ni kuwa makini darasani, kufanya mapitio ya masomo mara kwa mara, nidhamu na kujituma kwenye masomo na kumcha Mungu wakati wote.


Aliwapongeza walimu wa St Anne Marie Academy kwamba ni walimu wanaotambua wajibu wao kwani wamekuwa wakiwapa mitihani na mazoezi mengi hali ambayo imewaimarisha kitaaluma.


Mama mzazi wa Eluleki, Digna Mlengule aliliambia gazeti hili kuwa siri ya mtoto wake kuwa namba moja kitaifa kwenye matokeo ya darasa la saba mwaka huu ni juhudi zake binafsi na walimu wa shule ya St Anne Marie Academy ya Mbezi Kimara kwa Msuguri Dar es Salaam.


Akizungumza na gazeti hili jana, Digna  alisema Eluleki  ambaye ni mtoto wa kwanza na wa pekee kwa sasa alikuwa na bidiii sana ya masomo na wala hakuwa anahitaji kusukumwa kujisomea wakati wote.


Alisema haule ni mtu mtulivu, anayejitambua na kufanya mambo yake kwa mpangilio na wala hashinikizwi kutimiza wajibu wake kwenye masomo.


“Kwenye suala la masomo hakunisumbua hata kidogo nakumbuka wakati anaanza pre unit tu hapo St Anne Marie ndipo alikuwa anasumbua ila kuanzia darasa la kwanza mpaka la saba amekuwa mtu ambaye anajua afanye nini bila kusukumwa,”


“Nawashukuru sana walimu wa St Anne Marie Acedemy maana amesoma pale miaka yote 10 kuanzia chekechea, wamenipa faraja kubwa sana nawapongeza walimu kwa jitihada zao,” alisema


Kuhusu kazi anayotaka kufanya baada ya masomo yake, Digna alisema mara kadhaa amewahi kumsikia Eluleki akisema kuwa anataka kufanya kazi ya kurusha ndege au kuwa mpelelezi kwenye idara nyeti.


Digna alisema kwa sasa Eluleki anasoma masomo ya kuingia kidato cha kwanza shule ya Marian Boys ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani ila atajadiliana na baba yake ili waone kama aendelee kwenye shule hiyo au wampeleke shule nyingine.This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post