Sabaya na wenzake kurejea mahakamani kesho

 Na Mwandishi Wetu, Arusha

ALIYEKUWA Mkuu wa Wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro nchini Tanzania, Lengai Ole Sabaya ambaye amehukumiwa miaka 30 gerezani, kesho Jumatatu tarehe 18 Oktoba 2021, atarejea tena Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kusikiliza kesi nyingine inayomkabili.

 Sabaya mwenye umri wa miaka 34 na wenzake sita, wanakabiliwa na kesi nyingine ya uhujumu uchumi katika Mahakama hiyo ambayo Ijumaa iliyopita ya tarehe 15 Oktoba 2021, ilimhukumu kifungo cha miaka 30 baada ya kumkuta na hatia.


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post