Rais Samia kufanya ziara Arusha

 *Atatembelea mradi wa maji Longido

* Ni mradi unaosimamiwa na Auwsa

Na Seif Mangwangi, Arusha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan anatarajia kuanza ziara ya kikazi Mkoani Arusha kuanzia Oktoba 16,2021.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela Rais Samia atapokelewa na uongozi wa Mkoa wa Arusha ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa.

"Mhe. Rais akiwa Mkoani Arusha atafanya ziara ya siku 2  katika miradi ya Maji( Jiji la Arusha na Longido), Hospitali ya Jiji na Kiwanda cha Nyama Longido,"Amesema Mongela.

Amesema Mhe. Rais Samia atafanya mikutano ya hadhara miwili katika Viwanja vya Sheikh Amri Abeid na kiwanja cha standi mpya Longido ambapo anatarajia kuzungumza na wananchi na kueleza mwelekeo wa Serikali ya awamu ya sita.

Mongella amewasisitiza wananchi wote kujitokeza katika mikutano hiyo ya hadhara ikiwemo kusimama  barabarani kumlaki ikiwa ni mara yake ya kwanza kufika mkoani Arusha tangu alipoapishwa kuwa Rais wa awamu ya sita wa Tanzania.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post