Rais Samia azindua kituo Jumuishi cha utoaji Haki Dodoma,

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia wakati wa uzinduzi  wa Jengo la Kituo Jumuishi cha Utoaji  Haki katika eneo la National Capital City, Jijini Dodoma.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiondoa Kitambaa kuzindua rasmi Jengo la Kituo Jumuishi cha Utoaji  Haki katika eneo la National Capital City, Jijini Dodoma leo tarehe 06 Oktoba 2021. Wa pili kulia ni Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma, Jaji Mkuu wa Zanzibar Othman Makungu, wa pili kushoto ni Waziri wa Sheria na Katiba Prof. Palamagamba Kabudi na Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikata Utepe kuzindua rasmi Jengo la Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki katika eneo la National Capital City Jijini Dodoma leo tarehe 06 Oktoba 2021. Wa pili kulia ni Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Juma, Spika wa Bunge Job Ndugai, Jaji Mkuu wa Zanzibar Othman Makungu wa pili kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Palamagamba Kabudi, Mkuu wa Mkoa Dodoma Antoni Mtaka. 


Baadhi ya viongozi pamoja na wageni waalikwa wakifatilia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa  Jengo la Kituo Jumuishi cha Utoaji  Haki katika eneo la National Capital City, Jijini Dodoma leo tarehe 06 Oktoba 2021.

  PICHA NA IKULU

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post