Manumbu Mwenyekiti mpya chama cha wenye Ualbino Shinyanga

Viongozi waliochaguliwa na wanachama wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa shirikisho la vyama vya walemavu Mkoa wa Shinyanga (Shivyawata)

 Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Wajumbe wa mkutano mkuu wa chama cha watu wenye ualbino (TAS) mkoa wa Shinyanga wamechagua safu ya viongozi wapya watakaokitumikia chama hicho kwa muda wa miaka mitano ijayo 


Nafasi zilizochaguliwa  ni mwenyekiti wa mkoa wa Shinyanga, katibu mkoa, mhasibu mkoa, wajumbe watatu na mjumbe mmoja mwakilishi ngazi ya mkoa kwenye Taifa ambaye ni mjumbe wa kamati  kuu wa TAS Taifa


Akitangaza matokeo msimamizi wa uchaguzi huo afisa ustawi wa jamii mkoa wa Shinyanga Lyidia Kwesigabo amemtaja ndugu Yunice Manumbu kuwa ndiye mshindi wa nafasi ya mwenyekiti baada ya kupata kura zote 13, huku akimtaja Sitta Gility kuwa mshindi wa nafasi ya katibu baada ya kupata kura 12 kati ya kura 13


Viongozi wengine waliochaguliwa ni Saada Mususa ambaye amechaguliwa kuwa mweka hazina wa mkoa pamoja na wajumbe wengine akiwemo Self Rahid ambaye amechaguliwa kuwa mjumbe wa mkutano mkuu wa TAS Taifa maada ya kupata kura 12 kati ya kura 13


Akizungumza baada ya Uchaguzi Mkuu wa Chama cha watu wenye ualbino mgeni rasmi Afisa ustawi wa Jamii Mkoa wa Shinyanga Lydia kwesigabo ametoa wito kwa jamii hasa Wazazi na walezi kuwathamini na kuwapa fursa na haki sawa watoto wenye ulemavu 


“Tusiwabague wala kuwanyanyasa watu wenye ualbino, walemavu kwa sababu ni binadamu kama sisi tuwashirikishe kwenye masuala mbalimbali ya kimaendeleo lakini tusiwafiche watoto wenye ulemavu hasa wazazi tuwape haki za msingi ikiwemo kuwapeleka shule na kuwapeleka kwenye vituo vya kutolea huduma kwa ajili ya kupata chanjo mbalimbali na matibabu mengine hatimaye tuwe na Taifa lenye afya”


Mwenyekiti wa shirikisho la vyama vya Watu wenye ulemavu SHIVYAWATA Mkoa wa Shinyanga Mwalimu Richard Mpongo amepongeza hatua ya Serikali kutambua na kuthamini kundi la wenye ulemavu kutokana na utoaji wa fursa mbalimbali ikiwemo  mikopo inayotolewa na Halmashauri

 

Mpongo ameeleza kuwa serikali imeendelea kushirikiana na shirikisho hilo kwa namna mbalimbali ambapo mpaka sasa tayari halmashauri zote za Mkoa wa Shinyanga zimetoa Mikopo kwa wenye ulemavu

Amewaomba watu wenye ulemavu kutumia fursa zinazojitokeza mbele yao ili kujiongezea kipato na kujikwamua kiuchumi huku akiiomba serikali kuanza kuvipatia ruzuku vyama vya watu wenye ulemavu


 “Niwaombe watu wenye ulemavu kwa ujumla watumie fursa tulizopewa na serikali ya chama cha mapinduzi CCM lakini pia na taasisi mbalimbali lakini tukuombe mgeni rasmi vyama vya watu wenye ulemavu vyote Tanzania havina ruzuku ukatusemee tupewe hata kama ni kidogo vyama hivi vinauhitaji zaidi ya vyama vingine”


Mkutano mkuu wa chama cha watu wenye ualbino mkoa wa Shinyanga umefanyika leo kwa mujibu sheria na kanuni za katiba chama cha watu wenye ualbinoTanzania ambapo  safu ya viongozi wapya waliochaguliwa watakitumikia chama hicho kwa muda wa Miaka mitano ijayo

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post