Kanisa la Anglikana lamfagilia Rais Samia, Askofu Mkuu asema ameruhusu uhuru wa kuabudu

 Na  Mapuli  Misalaba,  Shinyanga

 

Askofu Mkuu wa kanisa la Evangelistic Assembless of Gog Tanzania (EAGT) Dkt Brown Mwakipesile ameishukuru Serikali kwa kuruhusu Uhuru wa kuabudu kwa dini na madhehebu yote Nchini hali inayoifanya Tanzania kuwa kisiwa cha amani


Ameyasema hayo leo wakati wa Ibada Maalum ya kuweka wakfu jengo jipya la Kanisa la EAGT, lililopo Ushirika Makimbilio Healng Centre katika Manispaa ya Shinyanga,ambapo ameahidi kwamba kanisa hilo litaendelea kuhubiri amani na kuliombea Taifa liendelee kuwa salama


“Tunaishukuru sana serikali yetu ambayo imeruhusu watu wake kufuata imani jinsi wao wanavyotaka na uhuru wa kuabudu bila buguza isingekuwa lahisi kujenga jengo hili kama pasingekuwa na amani na utulivu tumejenga na leo tumekusanyika kwa amani kwa sababu ya nchi yetu inalinda amani ya nchi lakini pia kuwaruhusu watu wake kuwa na uhuru wa kumwabudu Mungu bila vurugu kwa kweli hii tunamshukuru Mungu sana kwa Rais wetu na serikali kwa ujumla” amesema  Dkt. Mwakipesile


Akizungumza kwa niaba ya Makamu wa Rais Dkt Philp Mpango,Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga  Dkt Philemon Sengati   Amesema Serikali inatambua Mchango wa taasisi za Dini katika utoaji wa huduma za kiroho na kimwili lakini pia katika maendeleo na ustawi wa Taifa. 


akiwa ameambatana na kamati yake ya viongozi mbalimbali ikiwemo kamati ya ulinzi na usalama Mkoa wa Shinyanga Dkt. Sengati amewaomba Viongozi wa Dini na waumini wote kuendelea kushirikiana, kupendana pamoja na  kuliombea Taifa la Tanzania ili liendelee kuwa la mfano kwa mataifa 

 

“Tuendelee kuliombea Taifa letu lakini kuyaombea mataifa mengine yaendelee kuiga mfano wa nchi hii madhehebu ya Dini yamelitoa Taifa letu mbali sana yameendelea kuimalisha misingi ya upendo, utu wema, nidhamu, uadilifu na uzalendo zaidi mshikamano ndani ya Taifa letu yanasaidia sana na sisi hayo tunayashuhudia katika nyakati ngumu viongozi wa dini na waumini wa Tanzania tuendelee kuonyesha umoja, ushirikiano, tupendane na mwenyezi Mungu ataendelea kutunusuru na kutuweka salama”


Kwa upande wake askofu wa kanda ya ziwa magaribu ambaye pia ni mchungaji wa kanisa la EAGT Ushirika Makimbilio Healng Centre Kata ya Ndembezi mkoani Shinyanga Raphael Machimu amewashauri wakristo na watumishi wa Mungu kuwa na imani katika jambo lolote la kimaendeleo 


“Ushauri wangu kwa wakristo wengine na watumishi wa Mungu kwamba imani niyamuhimu katika katika maendeleo yoyote cha kwanza ni imani katika Mungu kwa kuambatana na ushirikiano moyo wa kujitoa watu wakifanya namna hiyo maendeleo makubwa yatatokea”

 

Katika taarifa yake kwa mgeni rasmi Mwenyekiti wa Kamati ya ujenzi wa Kanisa hilo John Ntalimbo akisoma lisala  amesema ujenzi wa kanisa hilo ulianza rasmi mwaka 2003 na kukamilika Mwaka huu 2021 ambapo umegharimu kiasi cha Shilingi za kitanzania Millioni 825


“Kazi ya Mungu ya mahali hapa ilianza rasmi mwaka 1993 kwa maombi ya Askofu Raphael Machimu akiwa na washirika watatu mpaka sasa kanisa linawashirika 600 ujenzi wa kanisa hili ulianza mwaka 2003 shughuli zote hizi zimeghalimu jumla ya Shilingi za kitanzania Milioni 825

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post