Diamond ashinda tuzo msanii bora Afrika

MSANII wa muziki wa Tanzania, Diamond Platnumz ametwaa tuzo katika Kipengele cha Msanii Bora wa Mwaka Afrika 2021 (African Artist Of The Year) katika Tuzo za Ghana Music Awards zinazotolewa nchini Uingereza.

 

Diamond alikuwa anawania kipengele hicho na wakali wengine Afrika kama Burna Boy, Davido, Wizkid, Master KG, Fireboy, Patoranking, Sinach, Mercy Chinwo, Judikay na Teni.

 

Diamond hakuweza kuhudhuria hafla ya utoaji wa tuzo hizo kutokana na kuanza ziara yake ya muziki nchini Marekani hapo juzi ambapo atafanya shoo 11 hadi Oktoba 31, 2021

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post