Wakumbushwa kutofanya biashara hifadhi ya barabara

 Na  Mapuli  Misalaba,  Shinyanga

Meneja wa Wakala wa Barabara mijini na vijijini TARURA wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga  Mhandisi Salvatory  Yambi amewataka Wananchi kutofanya shughuli za kibinaadamu kwenye hifadhi ya Barabara ili kuepusha madhara mbalimbali ikiwemo uhalibifu wa miundombinu 

Injinia Yambi amesema kwa mujibu wa Sheria inayosimamia Barabara namba 13 ya Mwaka 2007 na kanuni zake za Mwaka 2009, ni kosa kisheria kufanya shughuli za kibinaadamu kwenye hifadhi ya barabara ikiwemo kilimo,kupitisha mifugo, kufanya biashara na shughuli nyingine za aina hiyo.


Amewataka wananchi kutii sheria za barabani ili kutunza hifadhi hiyo na kuepusha madhara mbalimbali ikiwemo uharibifu wa miundombinu hiyo ikiwemo kulima kwenye kingo za barabara, kwenye karavati na madaraja


Injinia Yambi amezishauri mamlaka zote za maji kuhakikisha zinaomba kibali TARURA ili kupewa taratibu za kupitisha mabomba yao,badala ya kufanya shughuli hiyo kiholela 


“tunashauri mamlaka zote za maji zinapotaka kufunga mabomba ya maji kwa Mwananchi ni vizuri kuomba kibali TARURA ili waelekezwe namna bora ya kupitisha miundombinu yao,bila kuacha athari zozote” ameeleza Yambi


 Amesema  ni utaratibu mzuri kwa yeyote atakayehitaji kufanya shughuli kwenye hifadhi ya barabara kuomba kibali  TARURA ili kupatiwa maelekezo ya kitaalamu ya namna bora ya kufanya shughuli yake

Amesisitiza Wananchi kutunza miundombinu ya Barabara ikiwemo mitaro kwani ni kosa kisheria kufanya hivyo na iwapo itabainika mhusika atachukuliwa hatua za kisheria,hivyo wanapaswa kutunza miundombinu hiyo ili waweze kunufaika nayo kwa muda mrefu kwa kuwa ni njia ya mawasiliano inayorahisisha ukuaji wa uchumi  “tutunze mitaro,waepuke kufanya shughuli zinazochangia kuziba kwa mifereji,wasilime kwenye karavati,tusilime kwenye madaraja,tuepuke kulima kandokando ya barabara,ameeleza injinia Yambi. 


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post