Shinyanga wajipanga kuirejesha Mwadui ligi kuu, wadau wachanga Milioni42

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Philemon Sengati

 Na  Mapuli  Misalaba,  Shinyanga

Mkoa wa Shinyanga umezindua kampeni maalum iliyolenga kuboresha na kuhakikisha inazirejesha kwenye  ligi kuu timu mbili za mkoa huu kwa kuanzia na timu ya Mwadui Fc ambapo leo zaidi ya shilingi Milion 42 zimepatikana kupitia changizo la kutunisha mfuko wa dharura

 

Changizo hilo limeratibiwa na mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Philemon Sengati ambapo limehusisha kamati za ulinzi na usalama Mkoa na Wilaya pamoja na wadau mbaimbali wa michezo Mkoani Shinyanga wakiwemo wafanyabiashara, makampuni yanayomiliki migodi katika wilaya za Shinyanga kishapu na kahama 


Dkt. Sengati amesema michezo ni sekta mtambuka katika ustawi wa maendeleo ya mkoa na Taifa kwa kuwa inamahusiano makubwa na Biashara, Uchumi na uwekezaji 


Amesema licha ya timu za mkoa wa Shinyanga Stendi United na Mwadui Fc kushuka daraja lakini serikali ya mkoa wa Shinyanga haijakata tamaa na kwamba itahakikisha inaendelea kupambana ili kuhakikisha inazirejesha timu hizo kwenye ligi kuu 


“Niendelee kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na amili jeshi mkuu Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutengeneza mazingira mazuri ya sekta za kimaendeleo ikiwemo biashara, uwekezaji katika maeneo ya viwanda lakini na sekta zingine za kimaendeleo ikiwemo michezo. Na leo tunaongelea michezo kwani ni ni sekta mtabuka kwa ustawi na mendeleo ya mkoa na Taifa letu la Tanzania michezo inauhusiano mkubwa na biashara, uchumi na uwekezaji”


“Tulikuwanazo  timu mbili miaka iliyopita ikiwemo Mwadui na Stendi United hizi zote zilikuwa zinashiriki kucheza ligi kuu nitumie fulsa hii kujipatia pole kwamba timu zetu zote zimeshuka daraja lakini muhimu kwa sasa ni kupambana ili kuweze kurejea katika ligi kuu na tunaweza mimi niwahakikishie nitakuwa msitari wa mbele kulipigania hili” 


Dkt. Sengati amesema ataunda bodi maalum itakayohusisha viongozi wa serikali pamoja na wadau wa michezo ambapo amesema mkoa utahakikisha unawekeza zaidi kwenye raslimali watu, fedha na ujenzi wa miundombinu bora ya michezo ikiwemo uwanja

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amesema baadhi ya viongozi wa timu wamekuwa wakihusika kuzihujumu timu hizo kwa kutanguliza zaidi maslahi yao hali iliyochangia kushuka daraja kwa timu hizo 


“Mimi huwa sipendi kupepesa macho nasema ukweli wanaotushusha chini ni viongozi wa timu hizo zilizoshuka daraja huo ndiyo ukweli tukiweza kuwasimamia hawa viongozi wakajua manufaa ya zile timu kusimama na kufanya vizuri zile timu zitafanya vizuri viongozi wamekuwa wakilegalega hawaangalii mafufaa ya timu wanaangalia maslahi yao  binafsi lazima sisi tuwaeleze ukweli tatutaki mchezo kwenye kuzifufua hizi timu ili zirudi kwenye ligi kuu lakini hatutaki mchezo wa kuanza kuuza mechi inatukatisha tamaa sisi mashabiki ili tuendelee kufurahi mchezo wa kuuza mechi waache”


Kwa upande wao wadau wa michezo walioshiriki katika kikao hicho kilichojadili namna bora ya kupeleka michezo mbele katika mkoa wa Shinyanga  wameunga mkono wazo la mkuu wa Mkoa huo huku wengine  wakimuomba mkuu wa Mkoa kusimamia vizuri suala la viongozi ili wezi na matapeli wasiendelee kurudisha  nyuma Mkoa wa Shinyanga katika upande wa michezo ambapo wamesema bodi itakayochaguliwa na mkuu wa Mkoa huyo ilenge kunyanyua sekta ya  michezo katika Mkoa wa Shinyanga

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post