Amkata mkono mke wake kwa wizi wa mapenzi

 Na  Mapuli  Misalaba,  Shinyanga

Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linamshikilia  Jacob Mwajenga mwenye umri wa miaka 35 mkazi wa bushushu katika Manispaa ya Shinyanga kwa tuhuma za kumpiga mke wake Debora Rwekama  na kisha kumkata mkono  wake wa kushoto  chanzo cha tukio kinasadikiwa kuwa ni wivu wa mapenzi

kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga George kyando amesema tukio hilo limetokea siku ya Alhamis Septemba 09,majira ya usiku katika mtaa wa Bushushu manispaa ya Shinyanga ambapo mwanaume huyo amedaiwa kumpiga mke wake sehemu mbalimbali za mwili wake na kwamba baada ya kupoteza fahamu alikatwa mkono wake wa kushoto


Kyando amesema kuwa mtuhumiwa baada ya kufanya tukio hilo alimbeba mwanamke huyo mpaka kituo cha polisi wilayani kahama ambapo alitoa taarifa kuwa wamepata ajali wakati wakiwa safarini.


Mwanamke huyo anayejulikana kwa jina la Debora Rwekwama mkazi wa Bushushu katika manispaa ya Shinyanga  mwenye umri wa miaka 34 amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama huku hali yake ikitajwa kuwa mbaya.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post