Agape Shinyanga yawafanyia karamu Pili na Grace kwa kufaulu vizuri

 Na Mapuli  Misalaba,  Shinyanga

Katibu tawala wilaya ya Shinyanga BONIFACE NCHAMBI amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii, kuwa na nidhamu pamoja na kufuata sheria na taratibu zote za shuleni ili kutimiza ndoto za maisha yao

Ameyasema hayo leo kwenye sherehe ya kumpongeza Pili Omary na Grace Mahona ambao ni wanafunzi waliofanya mitihani yao ya kidato cha sita mwezi  wa tano mwaka huu nakupata ufaulu wa juu katika shule inayomilikiwa na shirika la Agape Mkoa wa Shinyanga

Katibu huyo amewaomba wazazi  kutowakatisha masomo watoto wa kike na badala yake wawaache wasome ili watimize ndoto zao

“Nitoe wito kwa wazazi tuwaache watoto wasome kama unataka Ng’ombe ukimuacha mtoto akasoma utapata zaidi tubadilishe mawazo yetu tuwaache watoto wasome ili watimize malengo yao”

Nchambi amesema wanafunzi hasa wanaoendelea na masomo watimize wajibu wao huku akiwataka kuacha kujiingiza kwenye mahusiano ya kimapenzi na mwanaume

“Timiza wajibu wako kama ni kusoma shule soma kweli  usijiingize kwenye mahusiano ya kimapenzi na wanaume  usikimbie vipindi darasani soma ili ulete mafanikio kwenye familia na taifa kwa ujumla”

Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa shirika la Agape TETER AMANI amesema Pili Omary amepata ufaulu wa daraja 1.9 ambaye alikuwa anasom Historia, Kiswahili pamoja na Englishi HKL ambapo Grace Mahona amepata daraja 2.10 ambaye alikuwa anasoma Historia, Geograph na English HGL

Aidha Amani amezitaja baadhi ya changamoto zinazoikabili shule hiyo ikiwa ni pamoja na maji, madarasa hayatoshi, vyoo, nyumba za kulala pamoja na miundombinu siyo rafiki 

Ameiomba serikali kutatua changamoto hizo ili kuweka mazingira safi na wezeshi kwa wanafunzi na walimu wa shule hiyo inayomilikiwa na shirika la Agape Mkoa wa Shinyanga linalotetea haki za wanawake na watoto


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post