TIGO WAKABIDHI MAMILIONI KWA MSHINDI WA SOKA NA TIGO

 Na Mwandishi Wetu.

Kampuni namba moja ya Huduma za Kidigitali hapa Nchini Tigo imekabidhi zawadi ya Milioni Tano kwa Mshindi wa jumla wa SOKA NA TIGO msimu wa 13 Bwn. Hassan Mohamed Timbulo (52) mkazi wa Kilombelo, Morogoro.

Akizungumza baada ya kukabidhi zawadi hiyo Meneja Mauzo wa Tigo Ifakara Bwana Haji Khatibu amesema kuwa katika msimu huu wa 13 jumla ya washindi 204 wamejishindia zaidi ya Shilingi Million 24.
"Wateja wetu wanaweza kushiriki mchezo huu wenye lengo la kukuza ufahamu na mapenzi ya soka kwa kutuma neno SOKA kwenda 15670 au kupitia Website yetu, tunawahimiza wateja wetu waendelee kucheza maana unavyocheza zaidi ndivyo unavyojikusanyia pointi zaidi na kujiongezea nafasi ya kushinda zaidi".


Kwa upande wake Mshindi wa Milioni Tano za Tigo Soka awamu hii Bwana Hassan Mohamed Timbulo amewasihi Wateja wa Tigo na Watanzania kwa Ujumla kushiriki Mchezo huu mara nyingi wawezavyo maana inaweza kuwa njia mojawapo ya kutimiza malengo yao ya kimaisha.
"Pesa hii itanijenga zaidi katika shughuli zangu za Kilimo kwa kununua mashine ya kulimia " Aliongezea Bwn. Timbulo.
Kumbuka ili kuibuka Mshindi wa Mamilioni ya Fedha kutoka TIGO SOKA Tuma neno SOKA kwenda 15670 ujibu maswali rahisi kuhusu soka na uibuke mshindi.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post