RC MTAKA AKIPONGEZA CHUO CHA DODOMA VOCATIONAL TRAINING CENTRE KWA KUTOA UJUZI

 

MKUU wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka ,akizungumza na wahitimu katika Mahafali ya tano ya Chuo cha Dodoma,Vocational Training Centre kilichopo jijini Dodoma.

MKUU wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka,akisisitiza jambo kwa wahitimu wakati akizungumza nao katika Mahafali ya tano ya Chuo cha Dodoma,Vocational Training Centre kilichopo jijini Dodoma.

Mkuu wa Chuo cha Dodoma,Vocational Training Centre,Jemima Nchimbi,akisoma risali wakati wa Mahafali ya tano ya chuo hicho kilichopo jijini Dodoma.

Baadhi ya wahitimu wakifatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati akizungumza katika Mahafali ya tano ya Chuo cha Dodoma,Vocational Training Centre kilichopo jijini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka akikata keki wakati wa Mahafali ya tano ya Chuo cha Dodoma,Vocational Training Centre kilichopo jijini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka akilishwa keki na Mkuu wa Chuo cha Dodoma,Vocational Training Centre,Jemima Nchimbi wakati wa Mahafali ya tano ya Chuo cha Dodoma,Vocational Training Centre kilichopo jijini Dodoma.

Mkuu wa Chuo cha Dodoma,Vocational Training Centre,Jemima Nchimbi akiwa katika meza kuu na baadhi ya viongozi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati wa Mahafali ya tano ya Chuo cha Dodoma,Vocational Training Centre kilichopo jijini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka,akiwa na Mkuu wa Chuo cha Dodoma,Vocational Training Centre,Jemima Nchimbi pamoja na viongozi mbalimbali wakiwa meza Kuu wakati wa Mahafali ya tano ya Chuo cha Dodoma,Vocational Training Centre kilichopo jijini Dodoma.

MKUU wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka,akimsikiliza Kiongozi wa Wazee Bw.Ezekiel Chadwanga wakati wa Mahafali ya tano ya Chuo cha Dodoma,Vocational Training Centre kilichopo jijini Dodoma.

MKUU wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka,akisimikwa Wazee Bw.Ezekiel Chadwanga kuwa kiongozi wao wakati wa Mahafali ya tano ya Chuo cha Dodoma,Vocational Training Centre kilichopo jijini Dodoma

MKUU wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka,akipokea zawadi ya Mbuzi kutoka katika uongozi wa Chuo cha Dodoma,Vocational Training Centre mara baada ya kuhudhuria Mahafali ya tano ya chuo hicho kilichopo jijini Dodoma

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka akigawa vyeti kwa wahitimu mbalimbali kulia kwake ni Mkuu wa Chuo cha Dodoma,Vocational Training Centre,Jemima Nchimbi wakati wa Mahafali ya tano ya Chuo hicho kilichopo jijini Dodoma.

..........................................................................................

Na Alex Sonna,Dodoma

MKUU wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka amewataka vijana wa Mkoa wa Dodoma kuhakikisha wanakuwa na ujuzi ili kwendana na kasi ya Mkoa huo kuwa Makao Makuu ya Nchi.

Akizungumza leo,Julai 22,2021,katika mahafali ya tano ya Chuo cha Dodoma,Vocational Training Centre(Dodoma VCT)Mkuu huyo wa Mkoa amewataka vijana wa Mkoa huo kuwa na ujuzi ili kuzikimbilia fursa mbalimbali ambazo zitapatikana kutokana na Mkoa huo kuwa Makao Makuu ya Nchi.

“Wito wangu kwa vijana wa Mkoa wa Dodoma niwatake kuwa na ujuzi katika Makao Makuu ya Nchi niwatake kila mmoja apate ujuzi tumieni vyuo vya kati wazazi niwaombe watoto wapate ujuzi kama hajafaulu apate nafasi ya kusoma ujuzi wowote, Dodoma na Dunia tunayoiendea itakuwa na fursa nyingi lakini kama huna ujuzi utapishana na fursa

“Mtu anaenda Garage anakuwa ni msafisha vioo lakini baadae anajifunza umakenika baadae anajifunza udereva anakuwa dereva,vijana wengi ni bodaboda wewe (wahitimu) kuwa fundi bodaboda utakuwa umepata ajira lazima vijana mhakikishe mna ujuzi na kuna kozi zingine ni fupi tu,”amesema Mkuu huyo wa Mkoa.

“Dodoma ni Makao Makuu hivyo mnafaida mjiandae miradi inayokuja ikukute una ujuzi hapa ujenzi ni mkubwa sana kama unakaa nyumbani hakuna kibarua ni wewe tu,tumia fursa.Tunajenga hapo Msalato likiwanja likubwa kabisa wakikuuliza una ujuzi wewe upo tu tafuta ujuzi.

“Kama unakaa hapa usidhani unapoteza muda kuna siku utamkumbuka huyu mama wazazi viombeeni hivi vyuo vya ujuzi kama kuna mtu anakudanganya fundi amekosa ajira huyo anakudanganya.Kama unasoma ujuzi shikilia hivyo ninyi hamjapoteza na wazazi mliopo nyumbani usikae na mototo ambaye hana ujuzi.

“Nakuombea Madame kazi zote duniani tunaanzia chini kazi moja tu ndio unaanzia juu kwenda chini kazi hiyo ni kuchimba kaburi na hapa tumeanza.Endelea kusoma mazingira kozi gani utaziongeza ili washindane na tembelea vyuo vingine uone ambavyo wanavyo wewe huna na mitaala pamoja na walimu,”amesema

Mkuu huyo wa Mkoa pia amekitaka Chuo hicho kuongeza ubunifu pamoja na kozi mbalimbali ili watu wengi waweze kupata ujuzi ambao utasaidia kuondokona na changamoto ya ajira.

“Madame nakushauru sana ongeza kozi tujitahidi tuweke matangazo kwamba Chuo kinafundisha kozi hizi na hizi local radio zungumza uwaokoe watoto wa Dodoma,tukitaka vijana wa Mkoa huu wawe washindani tuwapeleke kwenye elimu zote ya darasani,ufundi,elimu dunia aghera.Dunia tunayoiendea tunahitaji maeneo ya namna hiyo nimeona kozi zako ongeza kozi ili watu wajifunze kuwe na ujuzi”amesema.

Pia,amewataka wanafunzi licha ya kujifunza masomo mbalimbali pia wanatakiwa kuwa wabunifu ili wanapomaliza masomo yao waweze kuajirika kirahisi.

“Mjifunze vyote ujuzi na ubunifu ukienda mahali kutafuta vibarua unakuwa umekamilika kwa kila kitu,tunapeleka umeme vijiji vyote vya Tanzania kule vijijini hakuna mafundi maana yake fundi ni wewe.Tunapeleka umeme na maji katika vituo vya afya bomba likiharibika au kuziba wewe ndio fundi,”amesema.

Kuhusiana na changamoto ya eneo la ardhi la chuo hicho,RC Mtaka ameutaka uongozi wa Chuo kwenda makao makuu ya kata ili kukutana na timu ambayo inazunguka Mkoa wa Dodoma kumaliza changamoto za migogoro ya ardhi.

“Nikuombe kama utatumia nafasi vizuri,wanalalamikiana waende makao makuu ya Kata ili waweze kulitatua.Nakuomba uwezekutumia nafasi hiyo kupata muafaka katika siku hizo 10 ambazo tumeziongeza kwani tulitenga siku 10 na tuliongeza siku 10 zingine,”amesema RC Mtaka.

Awali akisoma risala Mkuu wa Chuo hicho,Jemima Nchimbi amesema wanakabiliwa na changamoto kukosa eneo la kujenga chuo kutokakana na eneo walilolipata kukabiliwa na mgogoro.

Amezitaja changamoro zingine ni vijana kutokupata mikopo kwa kozi za ufundi stadi,uelewa mdogo wa wazazi kutambua kozi zote ni kwa ajili ya jinsia zote.

Amesema mafanikio ambayo wameyapata ni pamoja na kufundisha vijana 679 wa kozi fupi,kufundisha vijana wa kike na wa kiume kwa kozi ndefu zaidi ya 333 ambapo vijana 1002 wameweza kupata mafunzo ambapo asilimia 75 wameajiriwa na asilimia 25 wamejiajiri.

Vilevile,amesema wamefanikiwa wamefanikiwa kutoa mafunzo kwa kina mama zaidi ya 197 kwa kozi za ujasiriamali na baadhi yao wamefungua maduka na kuuza bidhaa walizojifunza kutengeneza.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post