CRDB BENKI YATOA MIKOPO YA KILIMO YA BILIONI 735 NCHINI

 

Mkurugenzi wa wateja wadogo na wakati wa Benki ya CRDB Boma Rabala kushoto akisaini mkataba wa makubaliano  kati yao na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Makao Makuu Hipoliti Lello kwa ajili ya  Bima ya Afya kwa wakulima baina ya Benki ya CRDB, NHIF na Vyama vya Wakulima wa Mkonge (AMCOS)Halfa ilifanyika wilayani Korogwe

Mkurugenzi wa wateja wadogo na wakati wa Benki ya CRDB Boma Rabala kushoto akibalishana mkataba huo
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Makao Makuu Hipoliti Lello mara baada ya kutiliana saini
Mkurugenzi wa wateja wadogo na wakati wa Benki ya CRDB Boma Rabala kushoto akibadilishana mkataba huo na
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Makao Makuu Hipoliti Lello mara baada ya kutiliana saini
MKUU wa Mkoa wa Tanga Adam Malima akizungumza wakati wa halfa hiyo kushoto ni Mkurugenzi wa wateja wadogo na wakati wa Benki ya CRDB Boma Rabala kulia ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe Basila Mwanukuzi
Mkurugenzi wa wateja wadogo na wakati wa Benki ya CRDB Boma Rabala akizungumza wakati wa halfa hiyo
MKUU wa Mkoa wa Tanga Adam Malima akisisitiza jambo wakati wa halfa hiyo kushoto ni Mkurugenzi wa wateja wadogo na wakati wa Benki ya CRDB Boma Rabala  na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe Basila Mwanukuzi
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Makao Makuu Hipoliti Lello akzungumza wakati wa halfa hiyo

BENKI ya CRDB imetoa mikopo ya Kilimo yenye thamani ya Bilioni 735 katika mwaka wa fedha 2020/2021 ili kuongeza tija kwenye uzalishaji  ambayo ni sawa na asilimia 43 ya mikopo ya Kilimo inayotolewa nchini.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa wateja wadogo na wakati wa Benki ya CRDB Boma Rabala wakati wa halfa ya utiliaji wa sahihi wa makubaliano ya Bima ya Afya kwa wakulima baina ya Benki ya CRDB, NHIF na Vyama vya Wakulima wa Mkonge (AMCOS)

Halfa ilifanyika katika Ukumbi wa Korogwe Executive na kuhudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga wa Tanga Adam Malima wakiwemo viongozi mbalimbali.

Rabala ambaye pia ni Mkurugenzi mwenye dhamana ya uendeshaji na usimamizi wa Matawi ya Benki hiyo ambaye katika halfa hiyo alimwakilisha Afisa  Mkuu wa Biashara wa benki ya CRDB kwenye suala hilo.

Alisema kati ya mikopo hiyo Bilioni 494 imelekezwa kwenye mazao makuu ya kimkakati hivyo kusaidia zaidi ya Amcos zaidi 472 kupata mikopo  kwa ajili ya kuongeza tija kwenye uzalishaji wa kilimo ambapo ni maeneo ya mikopo ya pembejeo ,maghala.

Aliyataja maeneo mengine iliyotolewa mikopo hiyo ni ujenzi wa viwanda vya kuchakata mazao,mikopo kwa ajili ya miradi ya ufuigaji,uwekezaji kwenye misitu na mazao yake hasa kwenye maeneo ya uvuvi.

Mkurugenzi huyo wa wateja wa kati na wadogo alisema katika mikopo hiyo kwa Tanga wamewekeza kwenye zao la Mkonge na wametoa mikopo yenye thamani ya Bilioni 7.6.

Alisema fedha hizo zilitolewa kwa wakulima wadogo kupitia kwenye vyama vya ushirika wanaounganishwa kwenye mifumo madhubuti ya kifedha kupitia mtandao imara wa benki yao na mawakala  na huduma zao za Simbanking.

Aidha alisema kwamba benki hiyo imekuwa mstari wa mbele kufufua ushirika kwa kuongeza mitaji na ili kuhuisha na kujenga ushirika imara na wameweza kutoa mtaji wa bilioni 3.2 kwa benki ya Kakoba na hivi karibuni walitoa mtaji wa Bilioni 7 kwa ajili ya Benki ya KCBL hiyo inawezsha kwa benki hizo za ushirika kuweza kupata mitaji inayofikia bilioni 10.2.

Hata hivyo alisema hayo ni makubaliano kubwa sambamba kwenye suala la ushirika kuhaikisha mambo yanasonga mbele huku akitoa wito kwa kuvikaribsha vyama vya ushirika kujiunga na benki ya CRBD kuweza kupata mazingira wezeshi .

Naye kwa upande wake  Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima ameshuhudia utiliaji wa sahihi wa makubaliano ya Bima ya Afya kwa wakulima baina ya Benki ya CRDB, NHIF na Vyama vya Wakulima wa Mkonge (AMCOS) alisema mpango huo ni kwa sababu unakwenda kuhakikishia uhakika wa matibabu wakulima.

Alisema mkulima mwenye uhakika wa afya yake ni jambo zuri kwa sababu kupitia mpango wa bima litawawezesha kunufaika na huduma za matibabu wakati wanapokuwa wakugua.

”Jambo hili ni nzuri kwa sababu linawahakikishia wakulima wa mkonge waliojisajili ndani ya Ushirika kupitia (AMCOS) kujiunga na NHIF kupata uhakika wa matibabu kwa kuwewezshwa na Benki ya CRDB”Alisema

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post